SIKU moja baada ya
Rashford kudokeza kuwa safari yake na Man Utd iko katika hatua za ukingoni,
taarifa zimebaini kwamba Muingereza huyo anapendelea kujaribu bahati katika
ligi ya Uhispania.
Uamuzi wa RĂºben Amorim
kuwaacha Marcus Rashford na Alejandro Garnacho nje ya kikosi cha Manchester
United kitakachocheza dhidi ya Manchester City Jumapili iliyopita umechochea
uvumi zaidi kuhusu mustakabali wa Rashford katika klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Alex Crook
wa talkSPORT, klabu ya Saudi Pro League Al Ittihad inafuatilia hali ya Marcus
Rashford baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Manchester United na Amorim.
Zaidi ya hayo, TBR
Football inaripoti kuwa vilabu nchini Saudi Arabia vinaendelea kuonyesha nia ya
kutaka kumsajili Rashford lakini fowadi huyo wa Manchester United ameweka wazi
kuwa hataki kuhamia Mashariki ya Kati.
James Ducker wa
Telegraph anaripoti kwamba ikiwa Rashford ataondoka Manchester United,
anapendelea kuhamia Uhispania.
Bado, ni vigumu
kufikiria klabu yoyote ya LaLiga itamlipa mshahara wake isipokuwa anataka
kukatwa mshahara.
Mark Ogden wa ESPN
aliripoti kwenye safu yake kwamba Barcelona haitampa fowadi huyo njia ya kuanza
kazi yake kwani timu hiyo ya Catalan haina pesa au hamu ya kumfuata Rashford.
Wakati huohuo, Chris
Wheeler wa Daily Mail anapendekeza United inaweza kukaribisha ofa za takriban
pauni milioni 40 kwa fowadi huyo.
Kwa upande wa Paris
Saint-Germain, Laurie Whitwell wa The Athletic anaripoti kwamba wababe hao wa
Ufaransa hawana nia na Marcus Rashford.
Kwa kuongezea, Melissa
Reddy wa Sky Sports anaongeza kuwa hakuna klabu zinazomlenga kwa sasa,
akionyesha wasiwasi kuhusu uchezaji wake, tabia ya nje ya uwanja, na mshahara
mkubwa.
Rashford aliweka wazi
kwamba yuko tayari kuondoka na kutafuta changamoto kubwa na wakati PSG wamekuwa
wakimfuatilia kwa muda mrefu, inaaminika kwamba Rashford hana nia ya kuhamia
Ufaransa.