KAKA yake Paul Pogba, kiungo wa zamani wa Manchester
United, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela, miaka miwili kusimamishwa,
baada ya kukutwa na hatia ya kujaribu kumtapeli mwanasoka huyo wa Ufaransa.
Mathias Pogba, ambaye pia alipigwa faini ya Euro
20,000 (Ksh 2,679,174),
ataepuka kukaa jela na badala yake atatumikia mwaka mmoja akiwa amevalia
bangili ya kielektroniki.
Wanaume wengine watano walipatikana na hatia ya
unyang'anyi na uhalifu mwingine, na walipokea hukumu kati ya miaka minne na
minane katika mahakama ya Paris siku ya Alhamisi.
Paul Pogba, 31, alisema "alilaghaiwa na marafiki
zake wa utotoni" ambao walimshikilia kwa mtutu wa bunduki mnamo 2022 na
kumtaka atoe €13m (£10.8m). Alisema aliwalipa €100,000 (£82,600).
Wakili wa Mathias Pogba, Mbeko Tabula aliiambia RMC
Sport hukumu hiyo ilikuwa "kali sana" na akasema "Nadhani
tutakata rufaa".
Washitakiwa wengine watano walipewa hukumu zifuatazo:
Roushdane K alipokea miaka minane, Boubacar C miaka minne, miwili
iliyosimamishwa, Adama C miaka mitano, Mamadou M miaka mitano, miezi 12
kufungiwa, na Machikour K miaka minne, mitatu iliyosimamishwa.
Mwaka jana, Paul Pogba aliiambia Al Jazeera kwamba
alikuwa amefikiria kustaafu soka kwa sababu ya jaribio la ulaghai.
"Kuna pesa lazima uwe mwangalifu," alisema.
"Pesa
hubadilisha watu. Inaweza kuvunja familia. Inaweza kuunda vita".
Mwanasoka wa zamani wa kulipwa Mathias Pogba
alichezea vilabu vikiwemo Partick Thistle, Wrexham, Crewe Alexandra na Crawley
Town.
Klabu yake ya mwisho ilikuwa Belfort nchini Ufaransa,
akiwaacha mwaka 2022.