MSHAMBULIAJI wa Al-Ittihad, Mfaransa Karim Benzema amekanusha uvumi ulioripotiwa Desemba mwaka jana kwamba anafikiria kustaafu kutoka soka la kulipwa mwishoni mwa msimu huu.
Benzema ambaye amezungumzia uvumi huo kwa mara ya
kwanza, ametaja tetesi hizo kama ujinga mtupu, akisisitiza kwamba mwili wake
bado upo ngangari kinoma kuendelea kucheza.
“Kutastaafu baada ya msimu huu? HAPANA. SI KWELI. Upuuzi mtupu
huo, nani kasema. Najisikia vizuri!", alisema Karim Benzema.
Mwezi Desemba mwaka uliopita, majarida mbalimbali ya soka Ulaya
yalifichua kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa anafikiria
kustaafu mwishoni mwa msimu huu.
Benzema alitatizika katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi
Kuu ya Saudia chini ya Nuno Espirito Santo baada ya kuondoka Real Madrid, hata
hivyo, mshindi huyo wa Ballon d'Or 2022 amepata mafanikio msimu huu huku
Al-Ittihad wakiongoza msimamo wa ligi dhidi ya Al-Hilal na Al- Qadsiah.
“Huku kandarasi ya Mfaransa huyo ikikamilika 2026, Benzema
amekuwa akifikiria juu ya mustakabali wake,” chanzo kimoja kiliripoti.
Kulingana na ripoti hiyo, Al-Ittihad wanatarajia Benzema
kutimiza mkataba wake lakini klabu hiyo haitajali iwapo mshambuliaji huyo wa
Ufaransa ataondoka 2025 kwa sababu mshahara wake wa karibu Euro milioni 100
(£82.9m/$104.9m) ungewapunguzia kiasi kikubwa cha pesa. mzigo wa kifedha.
Kulingana na ripoti ya Relevo, klabu ya zamani ya Benzema,
Real Madrid, ilikuwa imejipanga kuwa balozi wa klabu hiyo Mashariki ya Kati,
kutokana na mahusiano ambayo mshambuliaji huyo amejenga kwa miaka mingi katika
eneo hilo.