logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Changamoto zinazoikodolea Macho taasinia ya michezo nchini

Tunapozungumzia michezo ni nyanja ambayo imesheheni aina mbalimbali za michezo ambayo kwa jumla huwekwa kwa chungu kimoja

image
na Evans Omoto

Michezo06 February 2025 - 05:53

Muhtasari


  • Michezo kwa kiwango cha kawaida huwapa vijana nafasi nzuri ya kujiimarisha na kuvianika vipaji vyao katika angaa za kimatifa kwa kucheza vizuri na kupata ajira ya kudumu.

Michezo ni sanaa muhimu katika maisha ya binadamu kwa kuzingatia michezo huwa na tija kubwa na kuwapa wengi nafasi ya kujiimarisha kiviungo na vilele ni burudani ya kufurahia nchini.

Tunapozungumzia michezo ni nyanja ambayo imesheheni aina mbalimbali za michezo ambayo kwa jumla huwekwa kwa chungu kimoja kiitwacho michezo kwa kutaja tu mifano ya michezo hio ni soka, riadha,voliboli,mchezo wa pete, michezo ya ushindani wa kuogelea pamoja na mchezo wa miereka.

Kwa hivyo niruhusu niweze kuangazia michezo ya kandanda,riadha na ragibi katika historia ya Kenya michezo imekuwa katika viwango vya juu sana, jambo hili lilichochea serilali kutenga wizara maalum ya michezo ili iwe ikiangazia na kuwapa vijana ambao wana ari na uchu wa kusakata kabumbu nchini nafasi ya kukuza vipaji.

Michezo kwa kiwango cha kawaida huwapa vijana nafasi nzuri ya kujiimarisha na kuvianika vipaji vyao katika angaa za kimatifa kwa kucheza vizuri na kupata ajira ya kudumu katika maisha yao.Hapa nchini Kenya kuna aina mbalimbali za ligi kuanzia viwango vya kaunti hadi kiwango cha taifa.

Kutokana na kuwepo kwa ligi hizo ambazo huwapevusha vijana kwa kuinua talanta zao na kuwapa nafasi za kushiriki katika michezo hiii ili kujiepusha na kujingiiza katika masuala ya kihuni kama taifa bado hatujaekeza ifaavyo katika soka kuhakikisha kuwa tunanawiri na kufikia viwango vinavyohitajika kimataifa.

Tukipiga msasa soka yetu na riadha bado kuna mianya mingi ambayo inawakumba wachezaji jambo ambalo huwadunisha na kuwaacha wakiwa kama wana wakiwa ,ligi kuu za Kenya kuanzia ligi za mashinani utapata kuwa huko ndiko vipaji vinakozaliwa kulelewa na hatimaye kufikia kiwango cha kuchezea ligi kuu ya taifa.

Ligi pana ya taifa( super league),ligi kuu ya Taifa(kenya premire league) na ligi za viwango vya daraja za kaunti FKF CUP,FKF charity shield na Top 8 cup ni baadhi ya ligi ambazo zinawakuza vijana na kutwaa ubingwa kwa kushinda mataji, licha hayo yote bado kuna hatua za kufanya ili michezo yetu nchini iwe na ladhaa na iwavutie waekezaji.

Kuna changamoto nyingi ambazo zinaikumba taasinia hii ya michezo kwanza tukizungumzia uongozi mbaya,ufisadi ukosefu wa fedha, ubaguzi wa wachezaji miongoni mwa changamoto kadhaa hili suala la uongozi mbaya limeathiri soka yetu nchini na kusababisha soka yetu kutopiga hatua.

Ukosefu wa fedha hili limekuwa dondaa ndugu ambalo limeizamisha soka yetu nchini kwa sababu timu zipo zina ari ya kucheza bali hazina pesa za kufadhili vilabu na kuwalipa wachezaji kwa wakati jambo ambalo kwa madai ya mbali husababisha timu kujipata pabaya kwa kushiriki katika michezo ya kamari ili zipate hela.(match fixing)

Uongozi mbaya na usimamizi wa vilabu pia umeathiri sana soka ya Kenya jambo ambalo limeacha soka yetu katika uzi mwembamba ulio katika kiwango cha kukatika .Kama taifa tunajipanga kuwa mwenyeji wa mashindano ya CHAN mwaka huu na AFCON mwaka wa 2027 wito wangu kwa waziri wa michezo Salim Mvurya,raisi wa shirikisho soka nchini Hussein Mohammed pamoja na washikadau ni lazima wahakikishe kuwa tunakabiliana na changamoto hizi na kufaulu.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved