logo

NOW ON AIR

Listen in Live

FKF yamteua Francis Kimanzi kuwa mkurugenzi wa maendeleo ya soka nchini Kenya

Shirikisho la soka nchini Kenya FKF limemteua Francis Kimanzi kuwa mkurugenzi ya maendeleo ya soka.

image
na Japheth Nyongesa

Michezo13 March 2025 - 13:57

Muhtasari


  • "FKF ina furaha kutangaza kuteuliwa kwa Francis Kimanzi kama mkurugenzi mpya wa maendeleo ya soka.
  • Alihudumu kama meneja wa mpito wa Kenya kutoka mwishoni mwa 2024 hadi Machi 2025.

Aliyekuwa mkufunzi wa Harambee Stars Francis Kimanzi

Shirikisho la soka nchini Kenya FKF limemteua Francis Kimanzi kuwa mkurugenzi wa maendeleo ya soka.

Kwenye barua ya FKF Kimanzi ametajwa kama mtu mwenye uzoefu wa kutosha na ambaye anaelewa kiundani mpira wa Kenya na talanta changa.

"FKF ina furaha kutangaza kuteuliwa kwa Francis Kimanzi kama mkurugenzi mpya wa maendeleo ya soka. Francis Kimanzi ni kocha mwenye uzoefu mkubwa na historia kubwa katika soka la Kenya, hatua ya shirikisho inataka kuimarisha nguvu yake, talanta ya asili ya ndani, na kukuza ukuaji endelevu ndani ya mchezo," sehemu ya barua ilisoma.

"Tuna hakika kwamba uongozi na utaalamu wa Bw Kimanzi utakuwa na jukumu muhimu katika kuendeleza ajenda ya maendeleo ya yetu na kuunda mustakabali wa soka la Kenya," alisema katibu mkuu wa FKF Harold Ndege.

Francis Kimanzi mwenye umri wa miaka 49 ni kocha wa soka wa Kenya ambaye anasimamia klabu ya Wazito na aliwaki kuichezea soka ya klabu ya Mathare United kati ya 1994 na 2002, kabla ya kuwa mkufunzi.

Kimanzi aliteuliwa kuwa meneja wa muda wa timu ya taifa ya Kenya tarehe 11 Desemba 2008 baada ya kushikilia wadhifa huo kama mlezi tangu Mei 2008. Alifutwa kazi kutoka nafasi ya kocha wa timu ya taifa baada ya Kombe la CECAFA la 2008 mnamo Januari 2009 kwa sababu ya migogoro kati yake na wasimamizi wa soka la Kenya.

Baada ya mwaka mmoja wa kufundisha klabu ya Sofapaka, aliteuliwa tena kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya mnamo Novemba 2011. Mnamo Juni 2012 alifutwa kazi kama meneja wa Kenya pamoja na wafanyakazi wake wote wa kufundisha baada ya Kenya kushindwa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Baada ya kufundisha Tusker, alirudi Mathare United kama meneja mwaka 2015.  Mnamo Agosti 2019 alihusishwa na kurudi kwa timu ya taifa ya Kenya.  Alirudi katika timu ya taifa ya Kenya kama meneja mnamo Agosti 2019. 

Kimanzi amezungumza hadharani dhidi ya makocha wa kigeni barani Afrika. Mnamo Oktoba 2020, alifukuzwa kufundisha Kenya. Mnamo Novemba 2020 akawa meneja wa Wazito. 

Alihudumu kama meneja wa mpito wa Kenya kutoka mwishoni mwa 2024 hadi Machi 2025


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved