
KOCHA wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametaja kikosi chake katika kibarua chake cha kwanza tangu kuchukua mikoba ya ukufunzi wa Three Lions mapema mwaka huu.
Katika kikosi hicho, majina yaliyokuwa
yamesahaulika yamerejeshwa tena kikosini huku wachezaji machipukizi pia
wakipata wito kwa mara ya kwanza.
Mshambulizi wa Aston Villa Marcus
Rashford ni miongoni mwa majina makubwa ambayo yamekuwa yakiachwa nje na
mameneja wa awali.
Rashford aliichezea Uingereza mara ya
mwisho katika mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mnamo Machi 2024 lakini amekuwa
na kiwango kizuri tangu ajiunge na Villa kwa mkopo kutoka Manchester United
mnamo Januari.
Mlinzi wa Newcastle Dan Burn na Myles
Lewis-Skelly wa Arsenal wako kwenye mstari wa kucheza mechi zao za kwanza baada
ya kuitwa kwa mara ya kwanza.
England wanaanza kampeni yao ya kufuzu
kwa Kombe la Dunia la 2026 kwa michuano miwili kwenye Uwanja wa Wembley dhidi
ya Albania na Latvia siku ya Ijumaa, 21 na Jumatatu, 24 Machi mtawalia.
Rashford bado hajafunga bao katika klabu
ya Villa lakini ameshapiga pasi nne za mabao huku akitaka kurejesha maisha yake
ya soka.
Burn hajashiriki England katika kiwango
chochote lakini amekuwa mchezaji wa kawaida na wa kudumu kwa Newcastle.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32
anatoa uwezo wa kubadilika ikizingatiwa anaweza kucheza katikati ya safu ya
ulinzi au beki wa kushoto.
Lewis-Skelly, 18, alicheza mechi yake ya
kwanza ya ushindani akiwa na Arsenal mwezi Septemba lakini ameibuka kuwa
mchezaji muhimu The Gunners.
Amekuwa akicheza nafasi ya beki wa
kushoto lakini pia anaweza kucheza kiungo na amecheza mechi 25 msimu huu.
Kipa wa Burnley James Trafford na mlinzi
wa Liverpool Jarell Quansah pia wanatumai kushinda mechi zao za kwanza za timu
ya wakubwa.
Hiki hapa ndicho kikosi chote kwa
ukamilifu:
Makipa: Dean Henderson (Crystal Palace),
Jordan Pickford (Everton), Aaron Ramsdale (Southampton), James Trafford
(Burnley)
Mabeki: Dan Burn (Newcastle United), Levi
Colwill (Chelsea), Marc Guehi (Crystal Palace), Reece James (Chelsea), Ezri
Konsa (Aston Villa), Myles Lewis-Skelly (Arsenal), Tino Livramento (Newcastle
United), Jarell Quansah (Liverpool), Kyle Walker (AC Milan, mkopo kutoka
Manchester City)
Viungo: Jude Bellingham (Real Madrid),
Eberechi Eze (Crystal Palace), Jordan Henderson (Ajax), Curtis Jones
(Liverpool), Cole Palmer (Chelsea), Declan Rice (Arsenal), Morgan Rogers (Aston
Villa)
Washambuliaji: Jarrod Bowen (West Ham
United), Phil Foden (Manchester City), Anthony Gordon (Newcastle United), Harry
Kane (Bayern Munich), Marcus Rashford (Aston Villa, kwa mkopo kutoka Manchester
United), Dominic Solanke (Tottenham Hotspur)