logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu mambo yaliyopendekezwa kwa FKF na mwanachama wa NEC

"Napendekeza mambo haya yajumuishwe kwenye ajenda na iwapo yatawapendeza yaidhinishwe yote au baadhi yake," alisema.

image
na Japheth Nyongesa

Michezo25 March 2025 - 12:21

Muhtasari


  • Kuwe na ukweli na uwazi ulionakiliwa wa matumizi ya fedha zinazotoka au kuingia kwenye benki.
  • Afisi za kamati ya kitaifa kwa soka la wanawake ibuniwe na iwe na mamlaka kwa shughuli zote za soka la wanawake nchini.
FKF Officials
Mwanachama wa kamati ya kitaifa ya utekelezaji katika shirikisho la soka hapa nchini Kenya Robert Macharia ametoa mapendekezo kadha ambayo anataka yaidhinishwe na kamati hiyo.

Kupitia barua kwa wanachama wenzake amewataka wakumbatie mapendekezo haya katika mkutano wao ujao huku akiwa na matumaini kwamba mapendekezo hayo yataweka mpangilio mzuri katika idara ya michezo hasa soka.

"Kulingana na kifungu cha [38] 3 cha katiba ya shirikisho la soka, mimi Robert Macharia, mwanachachama aliyechaguliwa kati, napendekeza kwamba katika mkutano wa wanachama ujao mambo haya yajumuishwe kwenye ajenda ya siku na iwapo yatawapendeza yaidhinishwe yote au baadhi yake," aliandika mwanachama huyo wa NEC.

Baadhi ya mapendekezo muhimu yaliotolewa na mwanachama Macharia ni pamoja na:- 

Kamati zote za shirikisho la soka ambazo zimetwikwa jukumu la kusuluihisha mizozo ya ya soka kukubaliwa kuenndelea kufanya kazi yao kwa umakini bila mwingilio kutoka kwa ofisi ya rais wa shirikisho au sekritiareti bali wawaunge mkono.

Mwanachama yeyote wa kamati ya kitaifa ya utekelezaji awe akiteuliwa na wanachama na iwe sheria isipokuwa rais wa shirikisho na naibu wake.

Kuwe na ukweli na uwazi ulionakiliwa wa matumizi ya fedha zinazotoka au kuingia kwenye benki kutoka kwa afisi kuu shirikisho la soka nchini na ziwekwe wazi mbele ya kamati ya kitaifa kila mwezi.

Waajiriwa wote wa shirikisho la soka wakiwemo wenye viti mbalimbali, kamati za sheria, fedha na wanaofanya kazi kwenye ofisi mbalimbali waajiriwe kwa njia ya uwazi na nyadifa zinazoachwa wazi zichapishwe hadharani kwenye mitandao yote ya kijamii ya FKF.

Huduma zote ambazo zinafaa kufanyika kwa FKF kama vile zabuni zitangazwe hadhari kwa umma na kuchapishwa kwa magazeti angalau mawili pamoja na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii ya FKF.

Wanachama wote wa mkoa waliochaguliwa watengewe angalau shilingi 250 000 kila mwezi ili kushugulikia gharama zote zikiwa pamoja na kulipa kodi ya ofisi inayotumika na mishahara.

Kamati ya Kitaifa ya Utekelezaji katika kila mkoa iwe na usemi wa mwisho kwa shuguli zote za soka eneo lake pamoja na kufanya makubaliano na wadhamini.

Afisi za kamati ya kitaifa kwa soka la wanawake ibuniwe na iwe na mamlaka kwa shughuli zote za soka la wanawake nchini. Zihusishe mwenyekiti wa wanawake na vijana.

Bodi ya soka la wanawake iwe na benki zao ambazo mapato ya wanawake yatawekwa pamoja na misaada mbalimbali pamoja na wadhamini. Benki hizo ziwe chini ya uangalifu wa wenye viti angalu watatu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved