
KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amedai kwamba mbinu zake za uchezaji katika klabu ya Man Utd zinaonyesha mafanikio makubwa licha ya kupoteza mikononi mwa Nottingham Forest.
Huku kukiwa na mechi nane pekee za Ligi ya Premia kuchezwa,
Mashetani Wekundu wamo na pointi nane kutoka kwenye nusu ya juu ya jedwali na
nusu ya ushindi wao 10 wameupata dhidi ya timu hizo tatu zote ambazo
zinatarajiwa kushuka daraja.
"Nadhani tulidhibiti
mchezo, lakini tayari tulijua kwamba timu hii inaweza kufunga mabao bila ya
chochote. Kisha inapofunga, inabadilisha mchezo kidogo kwa kile wanachotaka.
Tulijaribu wakati mwingine tukiwa na nafasi nzuri, lakini katika tatu ya
mwisho, krosi ya mwisho, pasi ya mwisho - haikuwepo. Wakati hatuna hilo,
hatuwezi kufunga mabao. Lakini msimu huu ni kama hivyo. ... Tunahitaji kupata
matokeo bora katika safu ya tatu ya mwisho."
Mreno huyo ambaye amekuwa na mwanzo mgumu katika taaluma yake
ya kuifunza Manchester United alisisitiza kwamba hawezi jidanganya kwani wako
katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.
"Naona [maendeleo] kwenye mchezo. Sijidanganyi. Kila mtu
anaweza kusema anachotaka lakini naona baadhi ya mambo, lakini tunahitaji
kushinda michezo ili tuende kwenye mchezo unaofuata."
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba Amorim ameshinda mechi sita
pekee kati ya 19 za ligi akiwa kocha, huku United wakiangalia umaliziaji wao wa
kwanza mkiani tangu msimu wa 1989-90.
Mreno huyo alisikitika uchezaji wa wachezaji wake baada ya
kupoteza Jumanne, akidai kuwa 'walisaidia Forest kushinda pointi tatu'.