Mwanariadha Emmanuel Korir aondolewa kwenye mbio za mita 400 kwa kuanza vibaya

Korir hata hivyo atahusishwa kwenye mbio za semi fainali za mita 800 baada yake kuhitimu siku ya Jumamosi pamoja na Michael Saruni na Ferguson Rotich.

Muhtasari

•Korir ambaye alimaliza katika nafasi ya sita kwenye mashindano ya 2019 Word Championships aliondolewa nje ya mashindano ya kikundi cha nne baada yake kuanza kukimbia mapema kabla ya bastola ya kuashiria mbio kuanza kulia.

Image: HISANI

Mwanariadha Emmanuel Korir kutoka Kenya aliondolewa nje ya mashindano ya kuwania nafasi kwenye mbio za mita 400 yaliyofanyika Jumapili asubuhi kufuatia mwanzo mbaya.

Korir ambaye alimaliza katika nafasi ya sita kwenye mashindano ya 2019 Word Championships aliondolewa nje ya mashindano ya kikundi cha nne baada yake kuanza kukimbia mapema kabla ya bastola ya kuashiria mbio kung'oa nanga kulia.

Korir hata hivyo atahusishwa kwenye mbio za semi fainali za mita 800 baada yake kuhitimu siku ya Jumamosi pamoja na Michael Saruni na Ferguson Rotich.

Korir alikuwa na matumaini ya kufika fainali katika mbio za mita 400 na mita 800.