logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Kahawa ndio imenisaidia kushinda dhahabu katika mbio za mita 5000,'Sifan Hassan

Mwanamke huyo wa Uholanzi anajinadi kuweka historia katika mbio za mita 1500, 5,000 na ​​10,000.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri02 August 2021 - 16:06

Muhtasari


  • Sifan Hassan aliyeshinda mbio za mita ,5,000 za wanawake hatimaye azungumza

Sifan Hassan ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 ikiwa ni mara ya kwanza kwa Sifan Hassan kushiriki na kusema ana kila sababu ya kushukuru kahawa baada ya ushindi huo wa Jumatatu.

Mwanamke huyo wa Uholanzi anajinadi kuweka historia katika mbio za mita 1500, 5,000 na ​​10,000.

Mzaliwa huyo wa Ethiopia, Hassan, 28, alitimka mbio kwa kasi ya juu na kushinda kwa dakika 14 sekunde 36.79, lakini inaonekana alihitaji msaada kidogo akielekea kumaliza.

"Bila kahawa singekuwa bingwa wa Olimpiki", alisema kwa utani.Ratiba iliyokaribiana ya Hassan inamaanisha atakuwa amekimbia katika mbio mara sita za umbali wa wastani au za masafa marefu katika kipindi cha siku nane.Katika mbio za kufuzu za mita 1500 mapema Jumatatu, ilibidi apone haraka baada ya kuanguka punde tu baada ya kengele kupigwa lakini alijinyanyua upesi kutoka nafasi ya 11 aliyokuwa wakati huo na kufuzu katika nafasi ya kwanza.

"Siwezi kuamini. Ilikuwa mbaya wakati nilijikwaa. Wakati nilianguka chini na ikabidi niruke, nilihisi kama nilikuwa nikitumia nguvu nyingi. Sikuamini hisia katika miguu yangu. Nguvu zote zilionekana kuniishia", alisema."Nilikuwa nimechoka sana. Bila kahawa singewahi kuwa bingwa wa Olimpiki. Nilihitaji kahawa yote!".

Bingwa mara mbili wa ulimwengu wa Kenya Hellen Obiri alipata medali ya fedha baada ya kumaliza kwa 14: 38.36, huku Gudaf Tsegay wa Ethiopia akichukua shaba baada ya kukamilisha mbio hizo kwa muda was dakika 14: 38.87.Hassan ana muda kidogo zaidi wa kupona kabla ya kushiriki mbio yake inayofuata - nusu fainali ya pili ya mita 1500, ambayo inafanyika Jumatano.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved