Mwanariadha Abel Kipsang aandikisha rekodi mpya katika mbio za mita 1,500

Muhtasari
  • Mwanariadha Abel Kipsang aandikisha rekodi mpya katika mbio za mita 1,500
Image: Hisani

Abel Kipsang alivunja rekodi ya Olimpiki katika mbio za mita 1500,wanaume kwa kukimbia kwa muda wa 3:31:65 na kufuzu kuingia kwenye fainali ya mbio hizo.

Kipsang alikimbia kwa saa saa 3: 31.65 akiboresha alama ya awali iliyowekwa na bingwa wa zamani wa Olimpiki Noah Ngeny huko Sydney miaka ishirini iliyopita ya 3:32 07.

Nyota wa Norway Jakob Ingrebrigsten alimaliza wa pili mnamo 3: 32.13 wakati Josh Kerr wa Uingereza alikuja wa tatu mnamo 3: 32.18 na Adel Mechad wa Uhispania katika nne bora 3: 32.19 wakati Stewart Mcsweyn wa Australia alikuja wa tano mnamo 3: 32.54

Bingwa wa Dunia Timothy Cheruiyot alimaliza wa tatu katika kipindi cha  saa 3: 33.95. Charles Simotwo alikosa nafasi katika fainali baada ya kumaliza sita katika 3: 34.61.

 

 

 

Image: Hisani