Mwanariadha wa Kenya na bingwa wa mbio za nyika mwaka 2015 Agnes Tirop ameaga dunia

Muhtasari
  • Mwanariadha wa Kenya na bingwa wa mbio za nyika mwaka 2015 Agnes Tirop ameaga dunia
Agnes Tirop
Image: Hisani

Mwanariadha wa Kenya na bingwa wa mbio za nyika mwaka 2015 Agnes Tirop ameaga dunia.

Agnes ambaye aliiwakilisha Kenya katika #tokyoolympics alipatikana na majeraha ya kuchomwa na kisu kwenye tumbo nyumbani kwake Iten, kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Mazingira ya kifo chake bado hayajafahamika, Mwanariadha huyo nyota alikuwa ameshikilia rekodi ya dunia mwezi uliopita baada ya kushinda mbio za kilomita 10 baada ya kutumia saa 30:01 wakati wa hafla ya Adizero huko Herzogenaurach, Ujerumani.

Alimaliza wa nne mnamo 14: 39.62 katika mbio za mita 5,000 za wanawake, mbio zilizoshindwa na Mholanzi Sifan Hassan.

Polisi wameanzisha uchunguzi wa kifo chake.

Mengi yafuata;