"Nitarejea kukimbia hivi karibuni" David Rudisha ahakikishia Wakenya baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu

Muhtasari

•Rudisha alisema upasuaji wake uliendelea vizuri na kipandikizi ambacho amekuwa nacho kwa kipindi cha mwaka mmoja unusu kiliweza kutolewa.

A file photo of Olympic 800m champion and world record-holder David Rudisha.
A file photo of Olympic 800m champion and world record-holder David Rudisha.

Siku ya Jumamosi nyota wa mbio za mita 800 David Rudisha alifanyiwa upasuaji kwenye mguu wake wa kushoto kutoa 'implant' ambayo amekuwa nacho kwa muda.

Katika ujumbe wake ambao alichapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu, Rudisha alisema upasuaji wake uliendelea vizuri na kipandikizi ambacho amekuwa nacho kwa kipindi cha mwaka mmoja unusu kiliweza kutolewa.

Rudisha ambaye amekosekana sana uwanjani kwa kipindi cha miaka minne ambayo imepita ameeleza matumaini yake ya kurejea kwenye riadha.

"Nina furaha kwamba Jumamosi tarehe 20 nilifanyiwa upasuaji wenye mafanikio wa kuondolewa kwa implant kwenye mguu wangu wa kushoto ambao umekuwa hapo kwa mwaka mmoja na nusu uliopita. Angalau nitarudi kukimbia hivi karibuni!!!!" Rudisha aliandika kwenye ukurasa wake wa  Instagram.

Rudisha aliambatainsha ujumbe wake na picha mbili za xray zinazoonyesha 'implant' ambayo   alikuwa nayo kwenye mguu wake.

Mashabiki wa mwanariadha huyo ambaye ameshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 wameendelea kumtumia jumbe za kuonyesha upendo huku wakimpa motisha wa kurudi tena uwanjani.