(Video) Ferdinand Omanyala azidi kutamba katika mita 100

Muhtasari

• Omanyala alisajili muda bora zaidi katika bara la Afrika mwaka huu

Ferdinand Omanyala alimshinda Akan Simbine kunyakuwa taji la mita 100 katika kinyang'anyiro cha ubingwa nchini Afrika Kusini. 

Huku hayo yakijiri Rais Uhuru Kenyatta amempongeza mwanariadha Ferdinand Omanyala kwa kushinda mbio za mita 100 katika mashindano ya Athletix Grandprix 4 nchini Afrika Kusini siku ya Jumatano.