Ethiopia yatuma salamu za rambirambi baada ya mwanariadha wa Kenya kuuawa

Muhtasari

• Polisi wanasema kuwa mpenzi wake kutoka Ethiopia, aliyetajwa kwa jina la Eskinder Hailemaryam, ni mshukiwa mkuu na anatafutwa.

Image: AFP

Shirikisho la riadha nchini Ethiopia limetuma salamu za rambirambi kwa familia na marafiki wa mwanariadha wa Kenya Damaris Muthee Mutua, 28, baada ya kukutwa amefariki akiwa na majeraha ya kuchomwa kisu katika mji wa Iten nchini , maarufu kwa kituo chake cha wakimbiaji wa mbio ndefu.

Polisi wanasema kuwa mpenzi wake kutoka Ethiopia, aliyetajwa kwa jina la Eskinder Hailemaryam, ni mshukiwa mkuu na anatafutwa. Bado hajatoa maoni yake na inasemekana alitoroka Kenya.

Shirikisho la Riadha la Ethiopia lilimtaja Mutua kama ‘’mwanariadha shujaa’’.

Alizaliwa nchini Kenya lakini ameshindania Bahrain.

Polisi wanasema mwili wa Mutua ulipatikana "ukiwa katika hali mbaya " huko Iten.

Yeye ni mwanariadha wa pili wa kike kuuawa katika mji huo katika mwaka mmoja.

Mwaka jana, Wakenya walishangazwa na mauaji ya mwanariadha wa Olimpiki Agnes Tirop.

Mumewe bado yuko kizuizini na anakanusha mauaji.