'Usain Bolt hafiki level yangu,'Omanyala ajipiga kifua

Muhtasari
  • Omanyala anasema anaamini kuwa ana kasi zaidi kuliko mshindi wa medali nyingi za dhahabu za Olimpiki ambaye kwa sasa amestaafu ingawa analenga kushinda rekodi yake ya dunia
Ferdinand Omanyala
Ferdinand Omanyala
Image: HISANI

Mwanariadha wa mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala ameshikilia kuwa mwanariadha mstaafu Usain Bolt hawezi mshinda.

Akiwa kwenye maahojiano, Omanyala anasema anaamini kuwa ana kasi zaidi kuliko mshindi wa medali nyingi za dhahabu za Olimpiki ambaye kwa sasa amestaafu ingawa analenga kushinda rekodi yake ya dunia.

"Sahii ni noma alistaafu haniwezi sasa hivi tunalenga rekodi yake ya dunia (sekunde 9.58) lakini lengo langu ni kutumia sekunde 9.6 kisha sekunde 9.5 hatimaye na kukaribia rekodi ya Olimpiki ambayo ni sekunde 9.63," Omanyala alisema.

"Ninajisikia vizuri kwa sababu ina maana tunafanya kazi kwa bidii na kile tunachofanya mazoezi kinafanya kazi pia, kwa hivyo ninahisi furaha kuwa mtu mwenye kasi zaidi barani Afrika na tunaendelea kupanda ngazi."

Omanyala alifichua kwamba anafanya mazoezi kwa saa 9 kwa siku lakini kwa sasa, anafanya somo moja kwa siku na zaidi kupumzika kwa sababu anachukulia riadha kama kazi na hataki kuharibu mwili wake.

"Tuna michuano ya dunia inakuja katika muda wa wiki tatu kwa hiyo hilo ndilo lengo kuu tunalolenga kwa sasa, na michezo ya jumuiya ya madola baada ya hapo itakuwa mwisho wa msimu wa mwaka huu." Alisema.