Wakenya wafanya vizuri katika mbio za mita 800, 5,000 huko Oregon

Mkenya Emmanuel Korir akimwongoza Ferguson Cheruiyot Rotich kunyakua dhahabu na fedha katika Michezo ya Olimpiki ya 2020 Tokyo, Japan.

Muhtasari

•Katika mbio za mita 5000 za wanaume Jacob Krop alishinda  kwa saa 13:13.30. Jakob Ingebrigsten aliwekwa wa pili kwa 13:13.92 huku Luis Grijelva wa Guatemala akiwa wa tatu kwa dakika 13:14.04. Daniel Simiu aliwekwa nafasi ya sita katika 13:15.17 lakini bado akapita kama mmoja wa walioshindwa kwa kasi (q).

Mkenya Emmanuel Korir akimwongoza Ferguson Cheruiyot Rotich kunyakua dhahabu na fedha katika Michezo ya Olimpiki ya 2020 jijini Tokyo, Japan.
Mkenya Emmanuel Korir akimwongoza Ferguson Cheruiyot Rotich kunyakua dhahabu na fedha katika Michezo ya Olimpiki ya 2020 jijini Tokyo, Japan.
Image: STAR

Wanariadha watatu wa Timu ya Kenya Emmanuel Korir, Emmanuel Wanyoyi na Wycliff Kinyamal wamefuzu katika fainali ya mita 800 katika mashindano ya Riadha ya Dunia yanayoendelea Oregon.

Korir, bingwa wa Olimpiki alishinda kwa saa 1:45.38 huku bingwa wa Michezo ya Jumuiya ya Madola Kinyamal akiibuka wa pili kwa 1:45.49 huku Peter Bol wa Australia akiwa wa tatu kwa 1:45.55.

Bingwa wa dunia wa vijana chini ya miaka 20 Emmanuel Wanyonyi alifuzu na kushika nafasi ya tatu.

Alitumia saa 1:45.42. Slimane Mouala wa Algeria aliibuka wa kwanza kwa saa 1:44.89 mbele ya Marco Arop wa Kanada kwa saa 1:45.12. Mkenya mwingine, Noah Kibet alikosa fainali baada ya kushika nafasi ya nane.

Katika mbio za mita 5000 za wanaume Jacob Krop alishinda  kwa saa 13:13.30.

Jakob Ingebrigsten aliwekwa wa pili kwa 13:13.92 huku Luis Grijelva wa Guatemala akiwa wa tatu kwa dakika 13:14.04.

Daniel Simiu aliwekwa nafasi ya sita katika 13:15.17 lakini bado akafuzu.

Oscar Chelimo wa Uganda alishinda joto kwa dakika 13:24.23 akifuatwa na Grant Fisher wa Marekani dakika 13:24.44, bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 5000 Selemon Barega dakika 13:24.44 na bingwa wa dunia wa mbio za mita 10,000 Joshua Cheptegei kwa dakika 13:24.77.