(+video) Mwanariadha aomba radhi uume wake kutoka nje ya kaptura akiwa mbioni

Kutokana na aibu, mwanariadha huyo alimaliza wa mwisho katika mashindano hayo.

Muhtasari

• Alberto Nonino ni kijana mwenye umri wa miaka 18 ambaye ni kinda wa Italia aliyedhalilika baada ya uume kumwagika.

Mwanariadha kinda kutoka Italia, Alberto Nonino ana kisa cha kuelezea ambacho kwako kilitokea kama mkasa wakati wa mashindano ya riadha ya dunia ya washiriki chini ya umri wa miaka 20 yanayoendelea huko Colombia.

Mwanariadha huyo kinda alikuwa mmoja wa washiriki katika mbio za mita 400 mkasa ulimtokea pindi kipenga kilipulizwa na wakaanza kuzitimuka. Baada ya mizunguko michache, uume wake ulitoka nje ya suruali, jambo ambalo lilimlazimu kupunguza kasi na kuzingatia kuuficha uume wake kwa kutumia mkono, na hivyo kuathiri mbio zake.

Katika video ambayo imesambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii, mwanariadha Nonino anaonekana akijaribu kwa jitihada kubwa kuuficha uume wake huo uliojitoma nje ya kaptura mara kadhaa akikimbia, mpaka kumlazimu kupunguza kasi na kumaliza mio hizo kwa sekunde 51.

Alberto Nonino baadae alizungumzia kisa hicho kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alieleza yaliyojiri na kuwaomba mashabiki wake na mashabiki wa riadha kote duniani msamaha kwa aibu hiyo.

“Ninataka tu kuzungumza na nyinyi kidogo kuhusu kile kinachoendelea katika blogu na mitandao ya kijamii. Ninafahamu hali hiyo na ni wazi ilikuwa ajali. Ninajaribu kucheka juu yake sasa hivi, lakini nilihisi vibaya mara tu baada ya mbio,” Alberto Nonino aliandika kwenye instastoris zake kwa lugha ya Kiitaliano.

Wajuzi wa masuala ya spoti wanasema hiki si kisa cha aibu cha kwanza kutokea ulingoni kwani mwaka 2018, mwanadada Venus William katika mashindani ya mchezo wa vikapu shindano la French Open, alitokea na kaptura iliyofanana na Ngozi yake ya mwili na wengi kwa kutazama mara moja walikuwa wakidhani yupo uchi wa hayawani.