Kiatu cha Kipchoge kwenye maonyesho ya duka huko Berlin

Kiatu hicho kiliwekwa kwenye maonyesho ya duka la Nike Run Club

Muhtasari

•Kiatu hicho cha rangi ya machungwa cha AF%2 runners ndicho kiatu alichokuwa amevalia Kipchoge katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumapili.

Kiatu cha mwanariadha Eliud Kipchoge ambacho kiko kwenye maonyesho Berlin
Image: Caroline Mbusa

Kiatu cha mwanariadha Eliud Kipchoge ambaye alivunja rekodi ya mbio za marathoni siku chache zilizopita kimewekwa kwenye maonyesho kule Berlin.

Kiatu hicho kiliwekwa kwenye maonyesho ya duka la Nike Run Club jijini Berlin, Ujerumani siku mbili baaada yake kushiriki mashindano ya Berlin Marathon.

Kiatu hicho cha rangi ya machungwa cha AF%2 runners ndicho kiatu alichokuwa amevalia Kipchoge katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumapili.

Aliandika sahihi yake kwenye kiatu hicho cha Nike na maneno mengine ambayo ni ‘Hakuna binadamu aliye na mipaka' pamoja na rekodi yake ya 2:01:09 ili kukitambulisha kama kiatu alichovalia wakati wa mbio hizo.

Kipchoge aliwafurahisha wakenya wengi kwa kuandikisha rekodi mpya ya  2:01:09, ambao ni sekunde 30 chini ya muda alioandikisha 2019. 

Eliud Kipchoge kwenye maonyesho ya kiatu chake huko Berlin
Image: Caroline Mbusa

Mwanariadha huyo aliweza kukutana na watu kadhaa waliohudhuria maonyesho hayo na kusema aliamua kuwazawadi kiatu hicho ili kuwapa matumaini ya mwangaza wa riadha na pia wanariadha wengine,

“Nilikuwa na furaha na bashasha nilipoweza kukutana na wanashiriki wa Nikeberlin na pia kuwahamasisha watu wawe na ujasiri wa kuvuka mipaka yao ,”alisema.

“Wanadamu sasa wamepata kasi zaidi na viatu vyangu vya AF%2 ndivyo nitakavyowacha nyuma kwa minajili ya riadha zijazo,”alisema.

Baada ya kuivunja rekodi yake, mwanariadha huyo alisema kuwa amefurahi kuivunja rekodi hiyo yake na kuifanya iwe ya kasi bora.

Kipchoge aliwashukuru wanariadha waliompa moyo, tumaini na kumhamasisha kufanya vizuri kila wakati.