Hongera! Amos Kipruto anyakua dhahabu katika London Marathon

Kipruto alikimbia kwa dhamira kubwa na kuvunja kanda kumaliza kwa masaa 2:04:39.

Muhtasari

• Leul Gebresilase wa Ethiopia aliibuka wa pili kwa saa 2:05.12 huku mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki, Bashir Abdi kutoka Ubelgiji akifunga orodha ya tatu bora.

Amos Kipruto asherehekea na bendera ya taifa baada ya kushinda shaba wakati wa mbio za marathon za wanaume
Amos Kipruto Amos Kipruto asherehekea na bendera ya taifa baada ya kushinda shaba wakati wa mbio za marathon za wanaume
Image: REUTERS

Amos Kipruto aliibuka mshindi katika mbio za wanaume za London Marathon 2022 Jumapili, wiki moja baada ya Eliud Kipchoge kuiba vichwa vya habari mjini Berlin.

Mwanariadha huyo kutoka Kenya alikimbia kwa dhamira kubwa na kuvunja kanda kumaliza kwa masaa 2:04:39.

 Leul Gebresilase wa Ethiopia aliibuka wa pili kwa saa 2:05.12 huku mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki, Bashir Abdi kutoka Ubelgiji akifunga orodha ya tatu bora.

Akizunguka msururu wa mwisho kupita Kasri la Buckingham, Kipruto alichagua raundi ya mbali, lakini alikuwa tayari amepata ushindi.

Akifikia alama ya 40km, Kipruto alitumia 1:58:27 na wakati huo ilionekana kufikia muda wake bora, pamoja na rekodi ya mashindano hayo.

Hata hivyo, alikimbia kwa urahisi na uwezo bidii kubwa isiyoweza kupingwa, akiwaacha Gebresilase, Abdi na Kinde wakigombania pumzi nyuma yake.

Ni Gebresilase na Abdi pekee aliweza kushikamana na Mkenya huyo katika mwendo wake wa kasi huku kundi lililobaki likisahaulika.