DIPLOMASIA

Balozi wa Kuba amtembelea rais wa NOCK

Tergat alisisitiza haja ya Kenya na Kuba kufanya kazi kwa karibu.

Muhtasari

•Tergat alisema kuwa ziara ya balozi huyo inalenga kuhimiza Kenya na Kuba kushirikiana katika programu mbalimbali za michezo.

•Kuba inasifika kwa kutoa baadhi ya mabondia bora zaidi duniani.

Rais wa NOCK, Paul Target akimpokea balozi wa Kuba nchini Kenya Juan Manuel Rodriquez Vazquez, katika afisi yake huko Westlands, Nairobi mnamo Ijumaa.
Rais wa NOCK, Paul Target akimpokea balozi wa Kuba nchini Kenya Juan Manuel Rodriquez Vazquez, katika afisi yake huko Westlands, Nairobi mnamo Ijumaa.
Image: HISANI

Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Kenya (NOCK) itaendelea kutumia michezo kama njia ya kuanzisha ushirikiano mpya na kuimarisha uhusiano na mataifa mengine.

Rais wa NOCK, Paul Target alisema hayo baada ya kumkaribisha balozi wa Kuba nchini Kenya Juan Manuel Rodriquez Vazquez, katika afisi yake huko Westlands, Nairobi mnamo Ijumaa.

"NOCK inajitahidi kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa kupitia michezo. Tunawahimiza wanariadha wetu kuendeleza uhusiano wa karibu na wenzao kutoka mataifa mengine," Tergat alisema.

Tergat alisisitiza haja ya Kenya na Kuba kufanya kazi kwa karibu, akisema nchi zote mbili zinaweza kufaidika na uhusiano huo wa pande zote.

“Juan Manuel Rodriquez Vazquez, balozi wa Jamhuri ya Kuba leo ametutembelea kwa heshima katika afisi zetu,” Tergat alisema.

Tergat alisema kuwa ziara ya balozi huyo inalenga kuhimiza Kenya na Kuba kushirikiana katika programu mbalimbali za michezo.

"Kuba ina fursa nyingi kwa wanariadha wa Kenya ambao wanaweza kufaidika pakubwa kupitia programu za michezo kati ya nchi hizo mbili.

Kuba inasifika kwa kutoa baadhi ya mabondia bora zaidi duniani.