Eliud Kipchoge kushiriki mbio za Boston

Kipchoge alivunja rekodi ya dunia katika mbio za Vienna.

Muhtasari

•Hata hivyo, Kipchoge atakabiliana na baadhi ya washindi wa mbio hizo kama vile Evans Chebet na Benson Kipruto.

Eliud Kipchoge baada ya kushinda dhahabu usiku wa kuamkia Jumapili
Eliud Kipchoge baada ya kushinda dhahabu usiku wa kuamkia Jumapili
Image: HISANI

Bingwa wa dunia katika mashindano ya riadha, Eliud Kipchoge, kwa mara nyingine anatarajiwa kushiriki katika mbio za Boston, nchini Marekani.

Mwanariadha huyo mwenye miaka 38 amevunja rekodi za dunia kadhaa, ikiwemo kukimbia kilomita 42  kwa chini ya masaa mawili.

Siku ya Jumatatu tarehe 17, Kipchoge atashiriki tena katika mashindano ya kilomita 42 kwenye mbio za Boston. Kama kawaida, watu wengi wana imani kuwa atanyakua ushindi kwa kuwa bora zaidi katika  mashindano hayo.

Kipchoge kwa upande wake amekuwa akifanya mazoezi ya kujiboresha katika nyanda za juu za bonde la ufa.Kipchoge amefaulu katika mbio zisizo za kasi ikiwemo za  Olimpiki za Brazil ,2015 ,na Japan mwaka wa 2021.

Kipchoge aliimarisha rekodi yake ya dunia  hadi masaa 2:01: 09 mara ya mwisho alipokimbia katika jiji la Berlin, Ujerumani kutoka kwa rekodi ya 2:01 : 39 aliyoweka katika jiji lilo hilo miaka nne awali.

Kwa sasa, Kipchoge ameshinda mbio za London na Berlin mara nne, zote mara nne nne. Ameshinda pia riadha za Tokyo na Japan. Hata hivyo, Kipchoge atamenyana na baadhi ya washindi wa mbio hizo kama vile Evans Chebet na Benson Kipruto.