Mkenya Beatrice Chebet aliongoza watatu bora Afrika katika mbio za mita 3000 kwa wanawake huko Diamond League mjini Stockholm, Uswidi Jumapili.
Katika hali ngumu ya hewa alirekodi wakati wake bora wa msimu wa dakika 14 sekunde 36.52.
Waethiopia Lemlem Hailu na Medina Eisa waliibuka wa pili na wa tatu Ethiopia na kumiliki medali katika mbio za mita 1500 kwa wanawake, huku Freweyni Hailu akiongoza kwa muda wa 4:02.31.
"Ushindi ni mkubwa lakini ushindani haukuwa mzuri kutokana na hali ya hewa. Lakini tunapaswa kukabiliana na hali zote," Hailu amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema.
Mafanikio mengine ya Afrika ni pamoja na:
- Akani Simbine wa Afrika Kusini ameshinda mbio za mita 100 kwa wanaume
- Zakithi Nene wa Afrika Kusini ameshinda mita 400 kwa wanaume
- Djamel Sedjati wa Algeria ameshinda mbio za mita 800 kwa wanaume
- Huku Tobi Amusan wa Nigeria akishinda mbio za mita 100 kwa wanawake