logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanariadha marehemu Kelvin Kiptum ashinda tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2023

Wakati huo huo, tuzo za SOYA zilikuwa zinaadhimisha miaka 20 tangu uzinduzi wao

image
na Davis Ojiambo

Michezo02 March 2024 - 07:53

Muhtasari


  • • Tuzo ya marehemu Kiptum ilichukuliwa na Patrick Makau ambaye alielekea kwenye ukumbi akiwa na hisia nyingi.
Kelvin Kiptum

Wiki chache baada ya kuzikwa, mwanariadha wa mbio za masafa marefu, Kelvin Kiptum ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo za SOYA usiku wa kumakia Jumamosi Machi 2.

Hafla ya kutolewa kwa tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa KICC.

Kiptum alishinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume kwa mwaka 2023 huku Faith Kipyegon akishinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kike.

Tuzo ya marehemu Kiptum ilichukuliwa na Patrick Makau ambaye alielekea kwenye ukumbi akiwa na hisia nyingi.

 

Kwa upande mwingine, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa mpigo kwa Kipyegon kushinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kike, kufuatia msururu bora wa mbio katika miaka ya hivi karibuni.

Kiptum ambaye alipoteza maisha yake katika ajali ya barabarani Februari 11 pamoja na mkufunzi wake kutokea Rwanda anakuwa mtu wa kwanza katika historia ya tuzo za SOYA kupokezwa tuzo angali amekufa.

 

Wakati huo huo, tuzo za SOYA zilikuwa zinaadhimisha miaka 20 tangu uzinduzi wao na mwanzilishi Paul Tergat, ambaye ni mwanariadha mstaafu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved