Mkenya Peres Chepchirchir avunja rekodi ya mbio za London marathon

Tigst Assefa wa Ethiopia alikuwa wa pili huku Joyciline Jepkosgei wa Kenya akiwa wa tatu.

Muhtasari

•Chepchirchir aliandikisha muda wa saa mbili dakika 16 na sekunde 16 katika mbio hizo ambapo waliomaliza wanne bora walishinda rekodi pekee ya awali ya wanawake ya saa 2:17:01.

Peris Jepchirchir
Image: BBC

Bingwa wa Olimpiki Peres Jepchirchir wa Kenya amevunja rekodi ya pekee ya dunia ya wanawake katika mbio za London marathon.

Chepchirchir aliandikisha muda wa saa mbili dakika 16 na sekunde 16 katika mbio hizo ambapo waliomaliza wanne bora walishinda rekodi pekee ya awali ya wanawake ya saa 2:17:01 iliyowekwa na Mkenya Mary Keitany mnamo 2017.

Tigst Assefa wa Ethiopia alikuwa wa pili huku Joyciline Jepkosgei wa Kenya akiwa wa tatu.

Mkenya Alexander Mutiso Munyao alimshinda bingwa wa mbio za masafa marefu Kenenisa Bekele na kushinda mbio hizo upande wa wanaume kwa saa 2:04:01.