logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanariadha Lawrence Cherono akabiliwa na mashtaka ya utumizi wa dawa za kusisimua misuli

Lawrence Cherono anakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kusisimua misuli kwa mara nyingine.

image
na Davis Ojiambo

Michezo13 June 2024 - 07:11

Muhtasari


  • •Mwanariadha Lawrence Cherono anakabiliwa na mashtaka ya utumizi wa dawa aina ya trimetazidine,inayofahamika kusisimua misuli.
  • • Hii ni mara ya pili kwa mwanariadha huyo baada ya kupigwa marufuku Julai,2022

Lawrence Cherono ambaye ni bingwa  wa Chicago Marathon 2019 ,ameshtakiwa kwa utumizi wa dawa za kusisimua misuli na kitengo cha uadilifu cha riadha (AIU).

Katika taarifa kupitia ukurasa wa X  Jumatano 12,Juni 2024, shirika la kupambana na dawa za kusisimua misuli lilithibitisha kuwa bingwa huyo mara mbili wa Amsterdam Marathon ameshtakiwa kwa utumizi wa dawa ya kusisimua misuli.

Hii si mara ya kwanza kwa mwanariadha huyo kwani,Julai 2022, Cherono alipigwa marufuku kwa muda baada ya kupimwa kuwa na dawa inayofahamika kama trimetazidine.

Dawa hii inajulikana kuboresha matumizi ya moyo ya oksijeni, uwezekano wa kuwapa wanariadha faida isiyo ya haki kwa kuimarisha viwango vyao vya uvumilivu.

Cherono alikuwa ameratibiwa kuwakilisha Kenya katika mashindano ya dunia huko Oregon, pamoja na Geoffrey Kamworor na Barnabas Kiptum, ndoto ambayo kwa sasa imesitishwa.

Mwanariadha huyo alishiriki mbio zake za mwisho kule Boston Marathon mnamo Aprili 2022 ambapo alitumia muda wa takriban 2:07:21  akimaliza kwa nafasi ya pili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved