Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024: Tazama ratiba ya timu ya Kenya ya Julai 31 - Agosti 4

Timu ya Kenya kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 tayari imeanza kushindana.

Muhtasari

•Washiriki kadhaa wanaowakilisha Kenya tayari wamekamilisha michezo yao au kutolewa nje ya mashindano hayo.

•Timu zingine kadhjaa pia zinatarajiwa kuchuana katika wiki hii. 

Team Kenya
Image: HISANI

Timu ya Kenya kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 tayari imeanza kushindana huku washiriki kadhaa wakiwa tayari wamekamilisha michezo yao au kutolewa nje ya mashindano hayo.

Timu ya raga ya wanaume ya Kenya 7s, almaarufu Shujaa 7s ilikuwa za kwanza kupeperusha bendera ya Kenya kuanzia Julai 24, 2024 lakini kwa bahati mbaya ilitolewa kwenye mashindano hayo ikiwa nambari 9.

Michezo ya kuogelea bado inaendelea huku mshiriki wa mchezo wa Fencing anayewakilisha Kenya tayari ametolewa kwenye mashindano hayo.

Timu ya voliboli ya wanawake ya Kenya inaendelea kucheza hata baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Brazil siku ya Jumatatu. Wanatarajiwa kucheza dhidi ya Poland leo, Julai 31 kabla ya kumenyana na Japan Agosti 3 kumaliza mechi zao za pool B.

Timu zingine kadhjaa pia zinatarajiwa kuchuana katika wiki hii. Tazama ratiba ya matukio:

Agosti 1:

  • Mashindano ya matembezi ya kilomita 20 kwa Wanaume - saa 7.30 asubuhi

Agosti 2:

  • Mbio za wanaume za mita 1500 raundi ya 1 - saa 11.05 asubuhi
  • Mbio za wanawake za mita 5000 raundi ya 1 – saa 6.10pm
  • Mbio za kupeana vijiti za jinsia mchanganyiko za 4 * 400m raundi ya 1- 7.10p.m
  • Mbio za mita 800 za wanawake raundi ya 1- 7.45p.m
  • Fainali ya mita 10,000 kwa wanaume - 9.20 p.m

Agosti 3:

  • Mbio za mita100 za awali za wanaume - 10.35a.m
  • Mbio za mita 100m za wanaume raundi ya 1 - 11.45a.m
  • Fainali za mbio za kupeana vijiti za 4*400m - 9.00pm
  • Kuogelea kwa mita 50m kwa wanawake, Maria Brunlehner - 12.00pm
  • Mpira wa wavu wa wanawake (raundi ya awali) vs Japan - 2.00pm

Agosti 4:

  • Mbio za mita 3000 Kuruka viunzi Wanawake raundi ya 1 - 10.05p.m
  • Mbio za mita 400 za wanaume Raundi ya 1 1 - 7.05p.m
  • Mbio za mita 100 za Wanaume nusu fainali - 8 p.m
  • Mbio za mita 800 kwa wanawake Nusu fainali - 8.35pm
  • Mbio za mita 1500 za wanaume Nusu fainali- 9.10pm
  • Fainali ya mbio za mita 100 kwa wanaume - 9.50 p.m