Hisia kinzani wanariadha wazawa wa Kenya wakiwakilisha mataifa mengine kwenye mbio

Mwanariadha Wilfred Yavi, mzaliwa wa Kenya anayewakilisha Bahraini, alichukua ushindi katika mbio za kuruka viunzi na maji ya mita 3000 kwenye mashindano ya Olimpiki jijini Paris.

Muhtasari

•Baadhi ya mataifa ambayo yamekuwa yakiwachukua wanariadha wa Kenya ni  kama vile: Marekani, Bahraini, Ubelji, Israeli, Kazakhstan na mengine mengi.

•Mataifa kama vile Marekani, Ubelji na Israeli huwavutia mno wanariadha kufuatia miradi ya juu iliyotengwa kwenye spoti 

Winfred Yavi
Image: HISANI

Taifa la Kenya limekuwa likishuhudia wanariadha wake wakiwakilisha mataifa mengine katika mashindano ya olimpiki.

Kisa cha hivi punde kiliwaacha wengi vinywa wazi na kuwaduwaza wananchi wa Kenya wakati ambapo mwanariadha Wilfred Yavi, mzaliwa wa Kenya anayewakilisha Bahraini,  alichukua ushindi katika mbio za kuruka viunzi na maji ya mita 3000.

Aidha, mkenya mwenza Faith Cherotich aligubia medali ya shaba na kuzidi kuipa Kenya matumaini katika mbio hizo huku maswali na midahalo ikichipuka zaidi kuhusu hali ya spoti hasa riadha nchini Kenya wakati ambapo wananariadha wanaamua kuwakilisha mataifa mengine.

Hapo awali, tetesi kutoka majarida kadhaa, wanariadha hubadilisha uraia wao kuelekea mataifa mengine kufuatia uwepo wa ushindani mkali nchini Kenya, ukosefu wa vifaa bora vya mafunzo, na ukosefu wa motisha katika suala la bonasi na ustawi.

Vilevilevile, kumetokea mjadala kwamba baadhi ya wanariadha wa Kenya hupata mishahara midogo ikilinganishwa na mataifa mengine ambapo wanariadha hupokea kitita kikubwa cha ngweje kila wanaposhiriki.

Wanariadha hubadilisha uraia wao ili wapige hatua katika kutumia viwanja vyema vilivyokarabatiwa, kujitavutia riziki pamoja na kunyakua mishahara minono.

Changamoto ziko kwa Kenya kuwekeza kwa wanariadha wa ndani ili waweze kujiimarisha kiuchumi bila kulazimika kuhamia nje ya nchi kutekeleza hivyo.

Baadhi ya mataifa ambayo yamekuwa yakiwachukua wanariadha wa Kenya ni  kama vile: Marekani, Bahraini, Ubelji, Israeli, Kazakhstan na mengine mengi.

Mataifa kama vile Marekani, Ubelji na Israeli huwavutia mno wanariadha kufuatia miradi ya juu iliyotengwa kwenye spoti vilevile fursa murua iliyowekezwa kwa wanariadha hawa kujiendeleza kimaisha.

Zaidi ya hayo, Kenya iwekeze hela zaidi katika riadha na spoti nyingine ili hii iweze kuwatia shime wanariadha wa Kenya ili kuzuia visa vya wanariadha wa Kenya kuenda kuwakilisha mataifa mengine.