•Raia huyo wa Algeria, alimshinda bingwa wa dunia wa China, Yang Liu kwa uamuzi wa kauli moja kushinda kitengo cha uzito wa welter.
Imane Khelif alishinda medali ya dhahabu ya ndondi ya Olimpiki kwa wanawake mwaka mmoja baada ya kuondolewa kwenye Mashindano ya Dunia kwa kutokana na suala la ustahiki wa jinsia.
Ingawa mzozo wa ustahiki wa jinsia umegubika matukio ya ndondi mjini Paris, raia huyo wa Algeria, alimshinda bingwa wa dunia wa China, Yang Liu kwa uamuzi wa kauli moja kushinda kitengo cha uzito wa welter.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliingia ulingoni huku akishangiliwa na mashabiki wengi wa Algeria - ambao walipeperusha bendera zao za kijani, nyeupe na nyekundu.
"Ndoto yangu yangu imetimia. Nina furaha sana," Khelif aliiambia BBC.
"Nimejiandaa kwa miaka minane kufikia ufanisi huu. Nataka kuwashukuru watu wote nchini Algeria.
"Ninafurahia sana utendaji wangu. Mimi ni mwanamke mwenye nguvu."
Matokeo yalipothibitishwa, Yang aliinua mkono wa mpinzani wake hewani - tofauti kabisa na matukio baada ya pambano la ufunguzi la Khelif dhidi ya Angela Carini wa Italia.