Mshikilizi wa rekodi ya mbio za mita 1500 kwa wanadada Faith Kipyegon ameelezea furaha yake alipoteuliwa kuwa nahodha wa kikosi cha Kenya cha Olimpiki mjini Paris.
Kipyegon alishinda medali ya dhahabu katika mbio hizo kwa mara ya tatu mfululizo katika michezo ya olimpiki huku akiisaidia timu ya Kenya kumaliza ya kwanza barani Afrika na 17 ulimwenguni katika mashindano hayo.
Aidha Kipyegon alimaliza wa pili katika mbio za mita 5000 nyuma ya Sifan Hassan kutoka uholanzi na kutwaa nishani ya fedha .vile vile ,aliwaongoza wanariadha wengine chipukizi kama Emmanuel Wanyonyi aliyempiku mwanariadha kutoka Canada Marco Arop na kutwaa dhahabu.
Kipyegon alidokeza kua anafuraha si haba baada ya kushinda medali ya dhahabu mfululizo na ni kwa neema zake Mungu ,akiongeza kua ni jambo ambalo ambalo litawapa motisha wanariadha chipukizi siku za usoni.
Aidha aliongeza na kusema kua mwanawe ndiye nguzo kubwa na chanzo chake kufanya vizurikatika mbio izo na kwamba mwanawe alikua anafuatilia jambo ambalo lilimpa motisha.
Vinginevyo Kipyegon amesema haikua rahisi kwake kutetea taji lake kwani kulikua na ushindani mkali kutka kwa wanariadha kutoka uhabeshi na vilevile Kenya.Aidha alisema kua yeye alifukuzia sana historia ili wakwanza kushinda mashindano hayo mfululizo na kuandikisha historia katika mbio hizo kwa kuvunja rekodi yake.