logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bondia afariki baada ya kupigwa KO katika shindano la ndondi

Zimunya, 24, wa uzito wa Super bantam, alifariki siku ya Jumatatu, baada ya kuzimia wakati wa pambano lisilo la ubingwa siku ya Jumamosi.

image
na Radio Jambo

Habari05 November 2021 - 05:31

Muhtasari


• Zimunya, 24, wa uzito wa Super bantam, alifariki siku ya Jumatatu, baada ya kuzimia wakati wa pambano lisilo la ubingwa siku ya Jumamosi.

• Zimunya alipigwa makonde kadhaa kichwani kabla ya kubanduliwa nje katika raundi ya tatu ya pambano la raundi sita.

• Baba yake Zimunya, Samson, alikuwa bondia mahiri asiye wa kulipwa na alitarajia mtoto wake angebeba jina la ukoo na kuwa bingwa.

Maswali yanaulizwa kuhusu taratibu za usalama katika ndondi ya Zimbabwe kufuatia kifo cha Taurai Zimunya baada ya kupigwa katika pambano mjini Harare.

Zimunya, 24, wa uzito wa Super bantam, alifariki siku ya Jumatatu, baada ya kuzimia wakati wa pambano lisilo la ubingwa siku ya Jumamosi.

Ni mara ya kwanza kwa bondia kufariki nchini Zimbabwe kutokana na majeraha aliyoyapata ulingoni.

Lawrence Zimbudzana, katibu mkuu wa Bodi ya Kitaifa ya Kudhibiti Ndondi na Mieleka ya Zimbabwe (ZNBWCB), anasema kuwa mipango ya uchunguzi bado haijashughulikiwa.

"Kwa sasa tutaangazia mazishi, na kisha tuketi na kuangalia masuala," Zimbudzana aliambia BBC Sport Africa katika mazishi ya Zimunya Jumatano.

Taarifa iliyotolewa na ZNBWCB ilisema kuwa "taratibu zote muhimu za matibabu zilifuatwa na msaada wa dharura wa matibabu ulitolewa mahali hapo kabla ya kupelekwa hospitali".

Zimunya alipigwa makonde kadhaa kichwani kabla ya kubanduliwa nje katika raundi ya tatu ya pambano la raundi sita.

Aliyekuwa mkufunzi wake Tatenda Gada alihuzunika, akihisi nyota huyo alikuwa na uwezo mkubwa.

"Tumeopokonywa mojawapo ya matarajio yetu mazuri," Gada alisema. "Nilifanya kazi na Taurai kwa zaidi ya miaka minne - nilimtazama akistawi na alikuwa mmoja wa nyota wajao katika fani hii."

Baba yake Zimunya, Samson, alikuwa bondia mahiri asiye wa kulipwa na alitarajia mtoto wake angebeba jina la ukoo na kuwa bingwa.

Ndondi ilikuwa imerejea tu Zimbabwe baada ya vizuizi vya kupambana na janga la corona kulegezwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved