Mike Tyson amrushia ngumi abiria mwenzake ndani ya ndege baada ya kurushiwa chupa

Muhtasari

•Msemaji wa Jumba la ndondi la Hall of Famer alithibitisha kwamba Tyson alimpiga abiria mwenzake ambaye alimchokoza bila sababu.

Image: BBC

Bondia wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson amempiga ngumi abiria mwenzake katika ndege baada ya mtu huyo "kumrushia chupa ya maji," msemaji wa Tyson amesema.

Video iliyochukuliwa kwenye ndege hiyo inamuonesha Tyson akiwa ameegemea kiti chake huku akimpiga ngumi za mara kwa mara mtu ambaye hakuonekana.

Msemaji wa Jumba la ndondi la Hall of Famer alithibitisha kwamba Tyson alimpiga abiria mwenzake ambaye alimchokoza bila sababu.

Polisi waliwaweka kizuizini watu wawili kwa muda.

Mtu mmoja alitibiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Francisco kwa kuwa alipata majeraha kidogo.

"Hawakutoa ushirikiano kwa polisi kufanya uchunguzi zaidi," msemaji wa Idara ya Polisi ya San Francisco alisema katika taarifa.

Wote wawili waliachiliwa huru "kusubiri uchunguzi zaidi". Idara ya polisi haikubainisha jina la mhusika yeyote.

Shambulio hilo lilitokea kwenye ndege ya JetBlue Jumatano usiku, kabla ya kuondoka San Francisco hadi Florida.

Video - iliyochapishwa na TMZ - haioneshi ugomvi wote na chupa ya maji kurushwa haioneshi.

Kwa mujibu wa TMZ, Tyson alikuwa amekubali kupiga picha na abiria mwanzoni mwa safari hiyo. Lakini mwanaume huyo aliendelea kumsumbua Tyson, licha ya Tyson kumuomba atulie.