logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bondia barobaro kutoka Kilifi amtaka Karim Mandonga kwenye pambano

"Unawapa umaarufu Tanzania na huwapi umaarufu Kenya, unatuharibia jina" - Kashindo alisema.

image
na Radio Jambo

Habari09 March 2023 - 10:39

Muhtasari


• "Tuko hapa na tuko tayari tu kurusha ngumi ndio kazi yetu,” Kashindo alimwambia Mandonga. 

• Takribani miezi miwili, Mandonga alishinda pambano nchini dhidi ya bondia Wanyonyi jijini Nairobi.

Bondia wa pwani amtaka Mandonga kwa pambano

Mwanamasumbwi mmoja kutoka kaunti ya Kilifi iliyoko ukanda wa pwani ametoa changamoto kwa bondia kutoka Tanzania Karim Mandonga almaarufu Mtu Kazi kujitoma ulingoni kwa pambano dhidi yake.

David Kashindo, bondia mchanga katika kaunti ya Kilifi alimtaka Mandonga kukubali mwaliko wake na kukipiga kwenye mduara nay eye, akisema kwamba pambano ambalo anajitapa kushinda miezi michache iliyopita jijini Nairobi lilikuwa dhidi ya mshindani hafifu ambaye hakuwa ameshiriki mazoezi ya kurusha ngumi kwa muda mrefu.

“Mandonga ni mtu mwingine ambaye anajaribu kuwaghasi Wakenya, yule mshindani aliyepata ni mtu ambaye alikuwa nje ya mazoezi kwa muda mrefu sana kumaanisha hata yeyote aliyetazama mpambano ule anaweza sema kama anarusha miaka kadhaa nyuma. Unahitaji damu changa, tuko hapa, tuko tayari hii ndio kufa au kupona. Unawapa umaarufu Tanzania na huwapi umaarufu Kenya, unatuharibia jina, tuko hapa na tuko tayari tu kurusha ngumi ndio kazi yetu,” Kashindo alisema.

Pia bondia huyo alitoa wito kwa shirikisho la mabondia wa Kenya kuwapa vijana chipukizi nafasi ya kuliwakilisha taifa katika mapambano kama hayo yanayowahusisha wageni kutoka nje ya nchi.

“Shirikisho la Kenya kwa mabondia mnahitaji damu change, tupe tu nafasi, tupe sapoti na muone jinsi tutapeperushwa bendera ya taifa. Vipaji viko sana Kenya na shirikisho likifanya vizuri upande wake basi tutapeleka mchezo wa ngumi mbali sana,” alisema.

Takribani miezi miwili iliopita, Mandonga alikuwa na mpambano wa ndondi dhidi ya Wanyonyo wa Kenya ambapo Mtanzania huyo mwenye mbwembwe na kujitapa mno alimshinda Wanyonyi katika raundi ya 7 na kutumia ushindi huo kupepea kwenye mitandao ya kijamii kote Kenya na Tanzania kwa siku kadhaa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved