Sonko atoa msaada kwa timu ya ndondi ya Kenya ya wanaotumia viti vya magurudumu

Timu hiyo ambayo imekuwa ikiwasihi watu wenye mapenzi mema kushughulikia mahitaji na changamoto zinazowakabili wanariadha walemavu ilikuwa imeomba usaidizi kutoka kwa aliyekuwa Gavana sonko.

Muhtasari

• Sonko aliwatembelea katika kambi yao ya mazoezi katika Jumba la Kijamii la Shauri Moyo ambapo alitoa sare na viza.

Mike Sonko atoa msaada kwa timu ya ndondi ya wanaotumia viti vya magurudumu nchini
Mike Sonko atoa msaada kwa timu ya ndondi ya wanaotumia viti vya magurudumu nchini
Image: HISANI

Timu ya ndondi ya wanaotumia viti vya magurudumu ya Kenya ilipewa ahueni Ijumaa baada ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwatembelea Ijumaa.

Timu hiyo ambayo imekuwa ikiwasihi watu wenye mapenzi mema kushughulikia mahitaji na changamoto zinazowakabili wanariadha walemavu ilikuwa imeomba usaidizi kutoka kwa aliyekuwa Gavana sonko.

Ombi hilo lilitolewa wakati timu hiyo ikitarajiwa kusafiri hadi Poland kushiriki mashindano ya ngumi za kulipwa mwezi Juni mwaka huu.

Wakiongozwa na Mary Atieno wachezaji walikuwa wameomba msaada wa kuwawezesha kujiandaa kabla ya mchuano wa Juni.

Sonko aliwatembelea katika kambi yao ya mazoezi katika Jumba la Kijamii la Shauri Moyo ambapo alitoa sare na viza.

Timu hiyo pia ilipata punching bag ambayo itawasaidia katika kipindi hiki wanapojiandaa na michuano hiyo.

Mary alidai kuwa wamekuwa wakikodisha begi la kuchomwa kutoka kwa mfanyabiashara wa ndani.

Timu ina matumaini kwamba italeta dhahabu nyumbani.