logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Michezo ya Olimpiki 2024: Bondia wa Nigeria apatikana na dawa ya kusisimua misuli

Bondia huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya matokeo lakini uamuzi wowote hautakuja kwa wakati.

image
na Samuel Maina

Michezo29 July 2024 - 07:27

Muhtasari


  • •Ogunsemilore ameondola katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024  baada ya vipimo kuonyesha ametumia dawa ya kusisimua misili.

Bondia wa Nigeria Cynthia Ogunsemilore ameondola katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 baada ya kusimamishwa baada ya vipimo kuonyesha ametumia dawa ya kusisimua misili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mwanariadha wa pili kufeli mtihani wa dawa kwenye Michezo ya Paris.

Ogunsemilore alitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya Olimpiki siku ya Jumatatu katika kitengo cha kilo 60 cha wanawake lakini sasa ndoto yake imesitishwa kufuatia ukiukaji wa kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Shirika la kimataifa la kukabiliana na utumizi wa dawa michezoni linasema sampuli ya nje ya shindano ilikusanywa tarehe 25 Julai na siku mbili baadaye ripoti ilionyesha matokeo chanya kwa furosemide iliyopigwa marufuku ambayo inaainishwa kama dawa ya kusisimua misuli.

Mnigeria huyo alishinda dhahabu katika Michezo ya Afrika mjini Accra mwaka huu na pia ni mshindi wa medali ya Jumuiya ya Madola.

Bondia huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya matokeo lakini uamuzi wowote hautakuja kwa wakati kwa ili kumwezesha kushiriki mashindano ya sasa.

Matokeo ya Ogunsemilor yanamaanisha kuwa Nigeria sasa imesimamisha wanariadha kwa ukiukaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli katika michezo miwili ya Olimpiki kufuatia mwanariadha Blessing Okagbare kufanyiwa majaribio miaka mitatu iliyopita mjini Tokyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved