Klabu ya Lille inayoshiriki katika ligi kuu ya Ufaransa sasa inaendelea kuweka rekodi katika kombe la klabu bingwa ulaya baada ya kuzipiga klabu kutoka Madrid.
Lille iliwapiku vijana wa Athletico Madrid wakiwa ugenini mabao 3-1 katika kipute hicho cha kombe bingwa ulaya, siku ya Jumatano 23 Mwezi wa Kumi.
Mechi iliyopita katika kombe hilo, Lille iliwapiga mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid bao 1-0.
Kando na mechi hiyo ya Lille matokeo mengine katika kombe hilo ni kuwa;
- Barcelona 4-1 Bayern Munich
- Benfica 0-3 Feyenoord
- Man city 5-0 Sparta Prague
- RB Leipzig 0-1 Liverpool
- Salzburg 0-2 Dynamo Zagreb
- Young Boys 0-1 Inter Milan
- Atalanta 0-0 Celtic
- Brest 1-1 Bayer Leverkusen