logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arsenal ni hasimu mkuu, lazima tupate alama zote 3 – Arne Slot

Slot amesema kwamba kupata alama tatu kutoka kwa mpinzani ni muhimu kwa kuwa haijulikani ni timu gani itakuwa mpinzani mkuu katika mechi za mwishi mwisho wa msimu.

image
na Brandon Asiema

Football27 October 2024 - 12:52

Muhtasari


  • Slot amesema kwamba kupata alama tatu kutoka kwa mpinzani ni muhimu kwa kuwa haijulikani ni timu gani itakuwa mpinzani mkuu katika mechi za mwishi mwisho wa msimu.
  • Arteta amewataka mashabiki kujitokeza zaidi kushabikia timu yao ili kuwapa motisha vijana wake kupata ushindi dhidi ya Liverpool.

caption




Kocha wa Liverpool, Arse Slot amesema kwamba timu ya Arsenal ni mpinzani mkuu wa Liverpool, na ni lazima vijana wake wahakikishe wanachukua alama zote tatu katika mchuano wa Jumapili.


Akizungumza kabla ya mechi hiyo inayosubiriwa Zaidi na mashabiki wa soka duniani, kocha Slot amesema kwamba kupata alama tatu kutoka kwa mpinzani ni muhimu kwa kuwa haijulikani ni timu gani itakuwa mpinzani mkuu katika mechi za mwishi mwisho wa msimu.


Slot amesema kwamba anaamini kuwa timu ya Arsenal itakuwa mpinzani mkuu wa Liverpool katika kinyang’anyiro cha kutwaa kombe la ligi kuu Uingereza hivyo kitu cha msingi zaidi nu kupata alama wala si kupoteza.


“Katika hatua hizi za mwanzo mwanzo, hakuna anyejua ni nani atakuwa mpinzani mkubwa, lakini nadhani kwamba sisi aote tunajua kuwa Arsenal atakuwa mmoja wao na kupoteza alama kwao ama kuzipata dhidi yao, hiyo ni muhimu sana.”  Alisema Slot.


Kwa upande wa Arsenal waliopoteza mechi ya awali ya ligi kwa kukubali kichapo cha mabao mawili kwa nunge dhidi ya Bournemouth, inalenga kurejea kwa mbinu zake za ushindi Jumapili.


Kocha Mikel Arteta amewataka mashabiki kujitokeza zaidi kushabikia timu yao ili kuwapa motisha vijana wake kupata ushindi dhidi ya Liverpool.


“Jumapili, tunawahitaji ata zaidi, nina uhakika watajitokeza na tutazidi kupiga hatua.“  Alisema Arteta.


Timu ya Arsenal inakosa huduma za wachezaji Bukayo Saka, Riccardo Calafiori na Jurrien Timber ambao wanaugusa majeraha ya misuli ya paja, goti na misuli mtawalia.


Vile watakosa huduma za Martin Odegaard, Takehiro Tomiyasu na Kieran Tierney ambao pia wana majeraha pamoja na William Saliba aliyepata kadi nyekundu katika mchezo wa awali.


Liverpool nao watakosa huduma za Diogo Jota, Cornor Bradley na Alisson Becker.

Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 1:30 Jumapili usiku.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved