Baadhi ya kaunti zitalazimika kushiriki tena uchaguzi wa
kuwachagua viongozi kwenye shirikisho la soka nchini FKF, baada ya wagombea
kutoshana katika kura.
Uchaguzi huo uliofanyika Alhamisi katika matawi mbali mbali
kote nchini, ulishuhudia kuahrishwa kwa mchakato huyo katika baadhi ya kaunti,
bodi ya uchaguzi wa FKF ikitarajiwa kuweka wazi tarehe ambazo uchaguzi huo
utaandaliwa.
Aidha katika kaunti nyingine, uchaguzi utarudiwa kwa mara ya
pili baada ya wagombea kutoshana kwa idadi ya kura.
Bodi ya uchaguzi wa
FKF inaoongozwa na mwenyekiti Hesbon Owilla, imesema kuwa uchaguzi
katika kaunti kama vile Bungoma, Bomet, Elgeyo Marakwet, Kakamega, Embu, Narok,
Samburu, Kisii, Lamu, Nandi na West Pokot kati ya nyingine zilikamilisha
uchaguzi wao vyema na washindi katika nyadhfa zilizokuwa zinawaniwa kuwekwa
wazi.
Uchaguzi katika kaunti za Turkana, Mandera na Homabay umeratibiwa
kufanyika siku tofauti.
Vile vile, baadhi ya matawi ya FKF yatalazimika kurudia uchaguzi baada ya wagombea kupata idadi sawa ya kura kwenye nyadhfa muhimu. Kaunti za Vihiga na Nyandarua ndizo zitarejelea uchaguzi wa nyadhfa hizo muhimu.
Katika kaunti ya Nyandarua, uchaguzi wa mwenyekiti na katibu mkuu wa tawi hilo utarudiwa Jumamosi baada ya wagombea wawili Reuben Kai na Charles Thotho kupata idadi sawa ya kura huku uchaguzi wa katibu mkuu katika kaunti ya Vihiga pia ukiratibiwa kurudiwa.
Uchaguzi za FKF kwenye ngazi ya kaunti zilihusisha mwakilishi
wa wanawake kwa FKF, mwakilishi wa vijana, mweka hazina, katibu mkuu wa kaunti
na mwenyekiti wa kaunti.
Wenyekiti waliochaguliwa katika kila kaunti, watashiriki
katika uchaguzi wa kumchagua rais wa shirikisho katika uchaguzi utakaondaliwa
Desemba 7.