Kocha wa Liverpool Arne Slot amekiri kuwa mechi ya Liverpool dhidi ya Southampton siku ya Jumapili itakuwa ngumu ligi ya Uingerza inapoingia raundi ya 12.
Akizungumza katika mahojiano na wanahabari Ijumaa mchana . kocha Slot amesema kuwa timu ya Southampton ina mtindo mzuri wa kucheza licha ya kutopata ushindi katika mechi za awali.
“Southampton wamekuwa na bahati mbaya lakini mtindo wao wa kucheza ni bora, wangeweza kupata matokeo katika kila mechi. Itakuwa mechi ngumu Jumapili.” Amesema Arne Slot.
Liverpool katika mechi kumi na moja ambazo wamecheza msimu huu, wameshinda mechi tisa chini ya kocha Arne Slot na kutoka sare mechi mbili pekee.
Kufikia sasa, timu hiyo inaongoza msimamo wa jedwali laligi kuu Uingereza kwa alama ishirini na nane, alama 5 mbele ya bingwa mtetezi Manchester City. Mpinzani wa Liverpool jumapili, Southampton yukokatika nafasi ya mwisho baada ya ushindi wa mechi moja na sare moja akiwa na alama 4.
Akizungumzia majeraha katika kikosi chake, kocha Arne amesema kuwa Virgil Van Dijk amerejea mazoezini na sasa yuko salama kucheza mechi ya Jumapili. Dijk amejiunga na wachezaji wenzake katika mazoezi ya Ijumaa ya matayarishoya mechi ya Jumapili.
Aidha, huduma za Trent Alexander-Arnold zikakosekana kwani kwa mujibu wa kocha Arne Slot
mchezaji huyo hajakuwa akishiriki mazoezi kutokana na jeraha lakini Slot
amesema kuwa mchezaji huyo atarejea hivi karibuni.