logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Simon Adingira na Ademola Lookman miongoni mwa wachezaji wa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa CAF 2024

Siku sita zimesalia kabla ya Afrika kutambua mchezaji, timu na mkufunzi bora wa mwaka katika hafla itakayoandaliwa nchini Morocco.

image
na OTIENO TONNY

Football13 December 2024 - 08:55

Muhtasari


  • Wachezaji watono wameteuliwa katika shindano la mchezaji bora barani Afrika.
  • Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilianza kutuza wachezaji bora wa soka kila mwaka  kuanzia mwaka wa 1992.


Shirikisho la soka barani Afrika lilianza kuwatuza wachezaji wa soka bora barani humo mnamo mwaka wa 1992.

Shirikisho hilo tayari limetoa orodha ya  wachezaji ambao wameteuliwa kwa mashindano hayo, wachezaji watano wameorodheshwa wakiwemo Simon Adingra ambaye ni mzaliwa wa Cote D’Ivoire mwenye umri wa miaka  22.Alizaliwa Januari mosi mwaka 2002. Mchezaji huyo anatumikia timu ya Brighton and Hove Albion inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza kama  mshambulizi.

Mchezaji mwingine aliyeteuliwa ni Serhou Guirassy mzaliwa wa Guinea mwenye umri wa miaka 28. Guirassy sasa anashiriki katika ligi ya mabingwa Europe akiichezea timu ya Borussia Dortmond kama mshambulizi katika msimu huu wa 2024/2025.

Mzaliwa wa Morocco na mchezaji wa klabu ya PSG. ni miongoni mwa walioteuliwa kwa shindano hilo. Hakimi ni mzaliwa  wa 4/11/1998 akiwa na umri wa miaka 26. Hakimi amezichezea vilabu za ughaibuni kama vile Real Madrid, Borussia Dortmond kwa njia ya mkopo, Inter Milan na sasa hivi anaiwakilisha klabu ya P.S.G.

Ademola Lookman Olajade Alade Aylola vile vile ni miongoni ya walioteuliwa na CAF. Mzaliwa wa Uingereza wazazi wake wakiwa ni raia wa Nigeria. Mchezaji huyo ameiwakilisha nchi ya Uingereza mpaka mwaka wa 2022 ambapo shirikisho la soka duniani lilikubali ombi lake la kuliwakilisha taifa lake la Nigera. Lookman aliichezea nchi ya Nigeria mara ya kwanza Mnamo tarehe 25 Machi 2022 katika mechi iliypokamilika kwa sare na timu ya Ghana. Mzaliwa huyo wa 20/10/1997 ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 27 anaichezea klabu ya Atalanta katika ligi ya Serie A.

Mchezaji anayefunga orodha ya wachezaji walioteuliwa ni Ronwen Williams raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa  miaka 32. Williams anachezea timu ya taifa ya Afrika Kusini kama mlinda lango na vile vile anaichezea timu ya Mamelodi Sundowns huku akiwa nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini pia.

Wachezaji walioshinda hapo awali ni pamoja na mchezaji wa Cameroon Samuel Eto'o ambaye aliibuka mshindi mwaka wa 2003, 2004, 2005 na 2010. Yaye Toure wa Ivory vile vile aliibuka mshindi kwa mara nne mtawalia kuanzia mwaka wa 2011 hadi mwaka wa 2014.

Siku zinasonga ikisalia siku sita ili kupata jina la wachezaji, wakufunzi na timu bora zaidi barani Afrika. Hafla hiyo itaandaliwa Marrakech nchini Morocco mnamo  Jumatatu  Disemba 16, 2024.


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved