logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Tunampenda Christo na tunamtaka hapa.” Enzo Maresca azungmzia Nkunku

Manchester United ilizingatia kumsajili mchezaji huyo katika majira ya joto, ingawa Red Devils hawakufanya mazungumzo rasmi.

image
na Brandon Asiema

Football26 December 2024 - 15:17

Muhtasari


  • Maresca amesema kwamba japokuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao hawana furaha na wengine wakitaka kuhama mwezi ujao, ana matumaini kwamba Christopher Nkunku sio moja wao


Kocha wa Cheslea amefichua kwamba mchezaji Chritopher Nkunku atasalia klabuni hapo licha ya tetesi ya kuwa angeliondoka katima dirisha la uhamisho linalotarajiwa kufunguliwa mwakani mwezi Januari.

Kocha Maresca amesema kwamba japokuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao hawana furaha na wengine wakitaka kuhama mwezi ujao, ana matumaini kwamba Christopher Nkunku sio moja ya wachezaji wanaowazia kuhama Chelsea.

“Kuna wachezaji ambao hawana furaha na wengine ambao wataomba kuondoka Januari. Sina hakika kama hiyo itakuwa kesi ya Christo ua mchezaji mwingine. Tunataka kuwaweka hapa.”  Alisema Maresca.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ufaransa amecheza jumla ya mechi 17 msimu huu akifunga mabao 10 licha ya kuwa amekuwa akiingia kutokea kwenye benchi katika mechi nyingi la ligi kuu nchini Uingereza.

Jarida la Eurosport limeripoti kuwa Manchester United  ilizingatia kumsajili mchezaji huyo katika majira ya joto, ingawa Red Devils hawakufanya mazungumzo rasmi.

Aidha Telegraph iliarfifu kwamba kwenye msimu huu katika mashindano yote ambayo Chelsea inashiriki, Christopher Nkunku ameanzishwa mara saba, mara tano ikiwa katika ligi ya mashirikisho ya barani Ulaya na mechi mbili kwenye ligikuu Uingereza.

"Nkunku ameichezea Chelsea mechi saba: tano kwenye Ligi ya Mikutano ya Europa na mbili kwenye Kombe la Ligi, ambazo Maresca amezitumia vyema kama muda wa mechi kwa kile kinachounda timu B yake.”  Telegraph iliarifu.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved