Hapo jana Jumanne 14, Januari 2025 mechi kadhaa za ligi ya
Uingereza ziliishia sare huku timu ya Chealsea, Liverpool na Manchester city
wote wakiandikisha sare na kuokota pointi moja katika mechi hizo.
The blues hapo jana walichuana na timu ya Bournemouth katika uga wa Stamford bridge ambapo mchezaji cole palmer aliiweka chealsea mbele katika dakika ya 13.
Baada ya bao la Palmer Chelsea walipoteza nafasi kadhaa katika kipindi cha kwanza na kuwalazimisha kulipia wakati Justin Kluivert aliifungia Bournemouth bao la kwanza katika dakika ya 50 kupitia mkwaju wa penalti huku Antoine Semenyo akifunga bao la pili katika dakika ya 68.
Beki Reece James alifunga bao la pili kwa timu ya Chelsea kupitia mkwaju wa faul katika dakika ya 95 ya nyongeza na kuipa chealsea pointi moja katika sare hiyo.
Chelsea sasa wako katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 37 huku Bournemouth wakishikilia nafasi ya 7 na pointi 34. Chelsea watawakaribisha Wolves Ugani Stamford Bridge Jumatatu 20,Januari 2025, huku Bournemouth wakikaribishwa na Newcastle tarehe 18 Jumamosi Januari.
Nottingham Forest na Liverpool zilitoka sare ya 1-1 kwenye uwanja wa City Ground Jumanne jioni, huku kikosi cha Nuno Espirito Santo kikitoa ushahidi zaidi kwamba ni tishio kubwa katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.
Bao la 13 la Chris Wood kwenye Ligi Kuu msimu huu mwishoni mwa kazi nzuri kutoka kwa Anthony Elanga liliipa Forest bao la kuongoza la mapema mnamo dakika ya kumi ya mchezo.
Kabla ya kona katika dakika 66, Kocha huyo Mholanzi Arne Slot aliwatoa Andy Robertson na Ibrahima Konate na kuwaingiza Kostas Tsimikas na Diogo Jota.
Wachezaji hao wawili walioingizwa kama wachezaji wa akiba walizalisha bao wakati Tsimikas alipata mpira na kuleta crosi safi huku Jota akiitikia kwa kichwa na kufunga bao la kwanza la kwa timu ya Liverpool.
Liverpool bado inashikilia nafasi ya kwanza na pointi 47 huku Forest wanafuata kwa pointi 41. Nottingham Forest watacheza dhidi ya Southamptom Jumapili 19, Januari 2025 huku Liverpool wakichuana na Brentford Jumamosi 18, Januari 2025.
Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Manchester city walitoka sare ya mabao mawili dhidi ya Brentford ,City ilionekana kutawala mchezo huo baada ya Phil Foden kufunga bao la kwanza kwa dakika ya 66 na kuongeza ya pili katika dakika ya 78.
Licha ya kutawala na kushikilia mabao hayo mawili kwa karibu dakika 80 Pep alishtuliwa kwa dakika ya 82 na bao la Brentford la kwanza kutoka kwa Yoane Wissa na vilevile bao la CristiaN Norgaard katika dakika ya 92 ya nyongeza na kuiona mechi hiyo ikiishia sare ya 2-2.
Manchester City wanashikilia nafasi ya 6 wakiwa na pointi 35 huku Brentford wakishikilia nafasi ya 10 wakiwa na pointi 28.
Brentford itachuana na Liverpool ambao ndio wanaongoza katika jedwali ya ligi hiyo mnamo Jumamosi 18, Januari 2025 huku Manmchester City wakicheza dhidi ya Ipswich Town Jumapili 19 Januari 2025.
Huku idadi ya mechi 21 zimekaragazwa bado ushindani mkubwa unaendelea kujidhihirisha katika nafasi ya nne bora huku timu zikiachana na pointi kidogo Liverpool bado ikishikilia nafasi ya kwanza.