Harambee Stars itajua wapinzani wao katika kundi lao la
kufuzu kwa CHAN 2025 katika hafla itakayoandaliwa 15 Januari katika ukumbi wa
KICC Nairobi kuanzia saa mbili usiku, huku Kenya ikijiandaa kuandaa mchuano
huo.
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limepanga kuandaa droo ya michuano ya mataifa ya Afrika ya TotalEnergies Africa (CHAN) .
Tukio hili linatarajiwa kubainisha makundi ya michuano hiyo itakayoandaliwa kwa pamoja kati ya Kenya, Uganda na Tanzania.
Kenya, pamoja na Uganda na Tanzania, zitashiriki michuano ya kufuzu kwa kanda ya CECAFA ikiwa ni wao ndio watakuwa waandalizi wa michezo hizo.
Kenya, Tanzania, Uganda, Morocco, Guinea, Senegal, Mauritania, Niger, Burkina Faso, Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kongo, Sudan, Zambia, Angola na Madagascar ni miongoni mwa timu zilizofuzu kushiriki CHAN.
Droo hiyo ni muhimu kwa timu zote zitakazoshiriki kwani inaweka mazingira mazuri ya kushiriki katika mashindano hayo, ambapo ni wachezaji wa ligi za ndani pekee wanaruhusiwa kuwakilisha nchi zao.
Mashabiki na viongozi wa kandanda kote barani humu wanasubiri kwa hamu matokeo hayo ambayo itachagiza mkondo wa michuano hiyo na kuelekea kwenye kutambua mabingwa wa kandanda barani Afrika
Droo ya leo huenda ikashirikisha timu 17 ambazo tayari zimefuzu, Hapo awali, timu 19 zililengwa kushiriki huku mshindi wa taji hilo kwa sasa ni Senegal.
Tukio hilo linakuja siku moja baada ya bodi hiyo kutangaza kuahirishwa kwa mashindano hayo kutoka Februari hadi Agosti kwa sababu ya changamoto ya miundombinu hasa yanayotokana na ukarabati ambao unaendelea katika uga mbalimbali ikiwemo uga ya Kasarani sports Centre.
‘’Wataalamu hao wa ufundi na miundombinu wa shirikisho la soka Afrika (CAF) ambao baadhi yao wamejikita nchini Kenya, Tanzania na Uganda, wameishauri CAF kuwa muda zaidi unaitajika kuhakikisha miundombinu na vifaa vinakuwa katika viwango vinavyohitajika ili kuandaa mashindano ya CHAN,’’ Alisema rais wa CAF Patrice Motsepe.
Hii ni mara ya pili kwa michezo hiyo kuahirishwa. CHAN 2024 awali ilikuwa imepangwa kufanyika Septemba 2024 lakini ilisogezwa hadi kati ya Februari 1 na 28, 2025, kutokana na ukosefu wa viwanja vya mechi vinavyokidhi viwango katika baadhi ya nchi waandalizi, ikiwa ni pamoja na Kenya.
Magwiji watatu wa soka kutoka Kenya, Uganda, na Tanzania wamethibitishwa kushiriki sherehe hizo. Wakiwemo McDonald Mariga wa Kenya, Hassan Wasswa wa Uganda na Mrisho Ngasa wa Tanzania hii ikiwa ni droo ya makala ya nane ya shindano hilo.
Wasswa, Ngasa, na Mariga ambaye ni makamu wa rais wa FKF kwa sasa nchini Kenya na wenzake wametoa mchango nmkubwa katika ukuaji wa soka barani Afrika na kuleta mchango mkubwa vilevile katika nchi yao.
Wasanii ambao wanatarajiwa kutumbuiza watu wakati wa hafla hiyo ni pamoja na Bien wa Kenya, kikundi cha densi cha Uganda, Ghetto Kids na wanakwaya wa Kenya Kenya’s Own Red Choir.