“Sijakua na tamaa ya kutokuwepo kwa muda mrefu”
Nahodha wa chelsea timu ya wanaume Reece James amerejea katika uwanja akicheza kwenye ligi kuu ya Uingereza .
James aliifungia chelsea bao lililowafanya kupata alama moja dhidi ya wahasimu wao Bournemouth, alifunga kupitia free kick.
Kufikia sasa nahodha huyo amekosa mechi 21 katika mashindano yote kutokana na jeraha la misuli ya paja akifaulu kucheza mechi 5 tu pekee za ligi kuu uingereza msimu huu.
Alionekana mwenye furaha zaidi baada kupiga free kick hiyo na kufunga huku meneja wa timu ya taifa Uingereza Thomas Tuchel akimutizama.
“Ulikuwa wa upweke na kuudhi”. James alliambia shirika la habari la BBC kuhusu muda wake Akiwa inje.
“ Nina furaha sana kurejea uwanjani na kusaidia timu yangu”
“Matumaini ni kuwa sawa mpaka mwisho wa msimu,”
James amekuwa inje kwa muda kutokana na majera ya goti na harmstring kwenye misimu kadhaa iliyopita.
Tangu James kuteuliwa kuwa nahodha wa chelsea, ameanizishwa tu kwenye michezo nane yenye michuano mikali.
Mara ya mwisho kuonekana alicheza dakika nane tu pekee dhidi ya Arsenal mwezi novemba huku akifunga bao lake la mwisho mwezi Oktoba 2022 dhidi ya AC Milan.
James mwenye uraia wa Uingereza alirejea uwanjani Jumapili baada ya kukaa nje kwa muda wa miezi miwili akicheza dhidi ya Morecambe kipindi cha kwanza pekee kwenye michuano ya kombe la FA.
James ambaye ameishindia timu yake ya taifa vikombe 16 aliulizwa kuhusu uwezekano wake wa kurejea kuichezea timu ya taifa na hili ndilo alilosema, “ Kwa sasa mkufunzi ni Thomas Tuchel na anaelewa uwezo wangu,”
James alikuwa na nafasi nzuri wakati Thomas Tuchel akiwa mkufunzi wa timu ya chelsea mwaka 2021 akiwa kwenye kikosi klichoishindia chelsea kombe la mabingwa ulaya huko German.