Bao la kujifunga la Dominic Solanke na ukamilishaji mzuri kutoka kwa Leandro Trossard iliipa Arsenal
ushindi baada ya Song Heung-min kufungia Tottenham bao la ufunguzi.
Arsenal walikaribia kufunga mwanya uliopo kati yao na vinara wa ligi kuu ya Uingereza Liverpool hadi pointi 4 baada ya ushindi huo wa 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya vijana wa Ange Postecoglou katika debi hiyo ya Kaskazini mwa London.
Kikosi cha Mikel Arteta kilikuwa kikihitaji sana matokeo mazuri ili kurudi katika fomu kufuatia kupoteza awali dhidi ya Newcastle na Manchester United wiki iliyopita, na kufanikiwa kupata ushindi mnono kwenye uwanja wa nyumbani ilionekana kuwapa matumaini The Gunners.
Son Heung-min aliifungia Arsenal katika dakika ya 25 na kuweka Tottenham mbele mpaka dakika ya 40 wakati Dominic Solanke alipojifunga na kuipatia Arsenal ba la kwanza.
Dakika nne baadaye Martin Odegaard alimpakulia Leandro Trossard pasi safi iliyomwona mbelgiji huyo akicheka na wavu na kupelekea kipindi cha kwanza cha dakika 45 kuishia 2-1.
Kipindi cha pili kilikuwa kipindi kigumu la jaribnio kutoka upande zote mbili ila hakuna aliyeiona lango la mwenzake katika dakika hizo 45 huku hali ya mchezo ya Tottenham Hotspurs ilionekana kuimarika zaidi licha ya bahati kutosimama muda huo wote.
Arsenal sasa wanashikilia nafasi ya pili na pointi 43 wakiwa pointi 4 pekee nyuma ya Liverpool huku Tottenham Hotspur wakishikilia nafasi ya 13 wakiwa na pointi 24.
Arsenal wanapania kuendelea kuziba pengo kati yao na Liverpool huku Jumamosi 18, Januari 2025 watachuana na Aston Villa na kwingineko Hotspur watajaribu kuingia katika nafasi ya kumi bora katika jedwali wakati watachuana na Everton Jumapili 19 Januari 2025.
Kufikia Januari 15, 2025, mechi 197 zimechezwa kati ya timu hizo mbili tangu mchezo wao wa kwanza kwenye Ligi ya Soka mnamo 1909, huku Arsenal ikishinda mara 84, ushindi wa 61 kwa Tottenham na sare michezo 52.
Arsenal imeweza kucheza mechi 59 dhidi ya Tottenham Hotspurs katika ligi ya Uingereza huku arsenal ikiitandika Totte mara 25 wakiwa nyumbani Fly Emirates na Tottenham ikiiadhibu mara 12 pekee wakiwa nyumbani katika uga wa Tottenham huku wakitoka sare mara 22.