Marcus Rashford yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kujiunga na Barcelona kutoka Manchester United, Real Madrid inakuwa klabu ya hivi punde zaidi kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Aston Villa Jhon Duran na Newcastle United wanapanga mkataba mpya wa muda mrefu kwa Alexander Isak.
Mshambulizi wa Manchester United Marcus Rashford, 27, yuko tayari kupunguziwa mshahara katika jaribio la kutaka kuhamia Barcelona mwezi Januari. (Daily Star Sunday)
Uwezo wa Barcelona kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Rashford unaweza kuimarika iwapo beki wa Denmark Andreas Christensen, 28, ataondoka klabu hiyo. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, huku winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, akihusishwa na uhamisho wa kwingineko. (ESPN)
Mkurugenzi wa Napoli Giovanni Manna amethibitisha kuwa klabu hiyo inavutiwa na mshambuliaji wa Garnacho na Borussia Dortmund Mjerumani Karim Adeyemi, 23, lakini akaongeza kuwa klabu hiyo ya Italia "haitalipa bei ambayo haiendani na thamani yake". (Football Italia, via DAZN)
Manchester United imekuwa na ofa nzuri zaidi ya pauni milioni 27 kwa beki wa kushoto wa Denmark Patrick Dorgu, 20, iliyokataliwa na Lecce, ambaye anataka pauni milioni 35. (Talksport)
Newcastle United inapanga kumpa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, mkataba mpya wa muda mrefu msimu wa joto. (Sunday Telegraph)
Madrid wameungana na Paris St-Germain na Al-Nassr kutaka kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 21. (Footmercato - in French)
Mshambulizi wa Slovenia Benjamin Sesko angependelea kuhamia Arsenal kuliko Chelsea au Manchester United lakini RB Leipzig hawataki kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 katika dirisha la uhamisho la Januari. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Aston Villa Emiliano Buendia anafuatiliwa na Bayer Leverkusen. Klabu hiyo ya Ujerumani inaangalia uwezekano wa kumchukua kwa mkopo na chaguo la kumnunua Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 28 lakini Villa wanataka kujumuisha kipengele cha kumnunua. (Sky Sport Germany)
Meneja wa Fenerbahce Jose Mourinho anataka kumsajili winga wa Barcelona Muhispania Ansu Fati, 22, kwa mkopo ili kuongezea timu nguvu ya kutwaa ubingwa. (AS - in Spanish)
Chelsea wamekubali ofa ya euro 12m kutoka Lazio kwa kiungo wa kati wa Italia Cesare Casadei, 22, katika mkataba unaojumuisha kipengele cha kuuzwa cha asilimia 25. (Sport Italia, via Football Italia)
Mshambulizi wa Lyon na Algeria Said Benrahma, 29, amekuwa akihusishwa na Ipswich Town lakini yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuhamia Neom SC, ambayo iko katika ligi ya daraja la pili nchini Saudi Arabia. (Footmercato - in French)