Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca akihutubia wanahabari ameweka wazi wachezaji ambao hawatakuwepo kutokana na majeraha.
Nicolas Jackson maamuzi ya kushiriki katika mchezo huo wa kesho Bado hayaamuliwa kutokana na jeraha alilopata usiku wa Jumatatu walipokuwa wakicheza dhidi ya West Ham United.
Jackson aliondolewa inje mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kupata jeraha la Hamstring. Mark Guiu ambaye aliingia nafasi ya Jackson pia hatakuwepo kutokana na jeraha alilopata mwishoni mwa mchuano.
"Marc ana jeraha baya kwa hivyo hatakuwepo. Huenda akawa nje kwa muda mrefu, tunangoja kujua muda kiasi gani labda wiki kadha. Nicolas anaeza kuwa sawa kabla ya mechi lakini kumuchezesha ni kuhatarisha, tutaona wakati huo, maumivu yake si makubwa. alieleza.
Walinzi Wesley Fofana na Benoit Badiashile wamekosekana kwa muda mrefu.
Enzo pia amethibithisha kutokuwepo kwa kiungo wa kati Romeo Lavia ambaye alikutana na majeraha yake wakati wa mechi yao dhidi ya Bournmouth mwezi jana.
"Romeo bado yupo kwenye harakati za kurudi ila bado ana mwendo mrefu mbele yake, alieleza Mkufunzi wa Chelsea Enzo.
Chelsea watakua wakicheza Kesho na Brighton & Hove Albion mwendo wa saa tano usiku kwenye kombe la FA mzunguko wa nne.
Brighton watakuwa wenyeji wa mchuano. mara ya mwisho mahaasimu hawa wawili kukutana huko Stamford Bridge , mchuano ulikamilika 4-2 kwa faida ya Chelsea.
Cole Palmer akifanikiwa kufungia Chelsea mabao yote manne huku Quomah Maleba na G. Rutter akizawazisha kwa upande wa timu ya Brighton.