logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Enzo Maresca azungumzia wachezaji wake kabla ya Chelsea kuchuana na Southampton Jumanne usiku

Mkufunzi wa timu ya Chelsea wanaume inayoshiriki ligii kuu ya uingereza, Enzo Maresca amezungumzia kikosi chake huku akiwa na imani ya kutwaa ushindi katika mchuano wa lJumanne usiku.

image
na Japheth Nyongesa

Football25 February 2025 - 12:09

Muhtasari


  • Maresca pia ameeleza kwamba kupoteza mchuano wa wiki jana dhidi ya Aston Villa haukumufurahisha na ilikuwa mojwapo ya siku mbaya kwake.
  • Kwa upande wake, Maresca ameelezea imani ya kutwaa ushindi kwa michuano yote iliyobaki kwenye ligii hiyo ya Uingereza.

Mkufunzi wa timu ya Chelsea, Enzo Maresca amezungumzia kikosi chake huku akiwa na imani ya kutwaa ushindi katika mchuano wa leo usiku Jumanne Februari 25.

Maresca akizungumza na wanahabari pia ameweka wazi wachezaji ambao hawatakuwa wakicheza usiku wa leo kutokana na majeraha.

Wanablues watakuwa wanawakaribisha mahasimu wao Southampton ambao wanashikilia nafasi ya mwisho kwenye jedwali katika ligii hiyo ya EPL.

Maresca pamoja na kikosi chake wanaamini kwamba huu ni mchuano ambao lazima wanyakue ushindi hasa kutokana kwamba wamepigwa nyumbani na ugenini kwa mechi tatu mfululizo kwenye michuano yote.

Kocha huyo akizngumza kuhusiana na majeruhi ameeleza kwamba, kwa upande wake mlinzi Travor Chalobah  hatakuwepo kwenye mchuano kutokana  na jeraha lake litakalochukuwa kati ya wiki moja na siku kumi.

"Alikuwa na ukaguzi jana na itakuwa karibu wiki moja au siku 10. Kwa upande mmoja ni vizuri kwa sababu sio jeraha kubwa na kwa upande mwingine, ni aibu kwa sababu tunampoteza mchezaji mwingine kwa wakati huu kutokana na idadi ya majeruhi tuliyonayo," alisema Maresca.

Mkufunzi huyo pia alioneka kutoridhishwa na kazi ya mlinda lango Filip Jorgenson katika mchuano uliopiata ila alikanusha madai kwamba anapanga kubadilisha mlinda lango wake wa kwanza katika mchuano wa leo.

"Yeye  yuko sawa. Anahisi huzuni kidogo, au kukasirika, kwa sababu anatambua kuwa kulikuwepo na kosa lakini kwa ujumla, yuko sawa." alisema akimurejelea Filip Jorgenson.

"Kama tunahitaji kubadilisha wachezaji kila wakati kuna makosa, tunahitaji kubadilisha wachezaji mchezo kwa mchezo, wachezaji wengi. Hapana, hakuna kilichobadilika," alizungumza Maresca huku akijitenga na kubadilisha mlinda lango.

Maresca pia ameeleza kwamba kupoteza mchuano wa wiki jana dhidi ya Aston Villa haukumufurahisha na ilikuwa mojwapo ya siku mbaya kwake.

"Hapana, bado nahisi hisia hiyo kwa sababu, utendaji ulikuwa mzuri sana kwenda Villa Park na kucheza kipindi cha kwanza tulichocheza ni taarifa muhimu. Tatizo la mwisho lilikuwa matokeo, matokeo hayakuwa mazuri kwetu. Ilikuwa ngumu wakati huo, pia kwa sababu tuko katika matokeo mabaya, kwa hivyo hiyo pia ndio sababu." Tunapaswa kufikiria juu ya michezo 12 ijayo." alieleza

Kwa upande wake, Maresca ameelezea imani ya kutwaa ushindi kwa michuano yote iliyobaki kwenye ligii hiyo ya Uingereza.

"Unapokuwa hapa Chelsea, huna michezo ambayo hujitayarishi kushinda. Wajibu wetu ni kujiandaa kila mchezo ili kushinda na kwa uhakika, kuanzia sasa, tukiwa na michezo 12 ya kwenda, hakuna shaka kwamba wote ni lazima washinde kwa ajili yetu." alikamilisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved