logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Enzo Maresca atilia shaka uwepo wa Palmer, James na Nkunku dhidi ya Copenhagen Alhamisi

Maresca akizungumza na vyombo vya habari aliaelezea kuhusu wachezaji na jinsi wanavyoendelea kupambana na majeraha

image
na Japheth Nyongesa

Football13 March 2025 - 12:10

Muhtasari


  •  Maresca amethibitisha kwamba Malo Gusto bado hayupo katika nafasi ya kucheza mechi ya Alhamisi pamoja na wachezaji wengine wa muda mrefu.
  • Alipoulizwa kuhusu Jackson, Mtaliano huyo aliongeza: "Anaweza kurudi baada ya mapumziko ya kimataifa, Noni pia. Hii ni habari njema."

Meneja wa Chelsea Enzo Maresca 


The Blues watakuwa wanawakaribisha wenzao wa Denmark Stamford Bridge Alhamisi ya leo jioni, wakitafuta kudumisha ushindi wao wa awali baada ya kushinda 2-1 kutoka kwa mchuano wa kwanza ili kufaulu kuweka nafasi katika robo fainali.

Kocha  mkuu Enzo Maresca akizungumza na vyombo vya habari aliaelezea kuhusu wachezaji na jinsi wanavyoendelea kupambana na majeraha yao.

Mkufunzi huyo wa Chelsea alieleza kwamba Cole Palmer, Reece James na Christopher Nkunku wote watafuatiliwa kwa umakini kabla ya mechi ya pili ya Ligii ya conference dhidi ya Copenhagen kwenye raundi 16.

"Kwa Cole, Reece na Christo, leo imekuwa siku ya kwanza [ya wiki]," Maresca alisema. "Jana hawakuwa hapa na siku mbili zilizopita tulikuwa na mapumziko. Leo tulishirikiana katika mazoezi, na tutaona kesho kama tunaweza kutumia baadhi yao."

 Maresca amethibitisha kwamba Malo Gusto bado hayupo katika nafasi ya kucheza mechi ya Alhamisi pamoja na wachezaji wengine wa muda mrefu Marc Guiu, Nico Jackson na Noni Madueke, ingawa raia huyo wa Italia ana matumaini kuwa wawili hao watarejea baada ya mapumziko ya kimataifa.

"Mchezaji mgeni ambaye bado amejeruhiwa ni Malo Gusto. Noni, Nico na wengine bado wako nje. Wengine wanaweza kucheza,'' Maresca aliongeza.

Alipoulizwa kuhusu Jackson, Mtaliano huyo aliongeza: "Anaweza kurudi baada ya mapumziko ya kimataifa, Noni pia. Hii ni habari njema."

"Sasa kabla ya mapumziko tuna michezo miwili, kesho na Jumapili, halafu tuna mapumziko ya kimataifa na tunaweza kupata nguvu, kurejesha wachezaji, na kisha kwenda kwa mbio za mwisho."

Maresca pia alieleza kuwa Romeo Lavia yuko sawa na atakuwepo siku ya Jumapili kwenye ligi kuu ya England kwenda Arsenal baada ya kuwa kwenye benchi dhidi ya Leicester City mara ya mwisho.

 "Romeo yuko bora zaidi. Hayupo kwenye kikosi cha Ligi ya conference kwa bahati mbaya lakini kwake ni sawa na kama Reece James  lengo kuu kwetu ni kuwasaidia kuwa sawa hadi mwisho na kuwawezesha kucheza mechi nyingi kadri wawezavyo."

 Maresca alipoulizwa kama atakwenda na Robert Sanchez - ambaye alicheza dhidi ya Leicester - au Filip Jorgensen, ambaye amecheza sana katika Ligi ya conference.

"Tutaona bado sijaamua na bado tuna saa 24 kabla ya mechi ya kesho. Kama nilivyosema awali, tuna makipa wawili wazuri  Rob na Filip, na tutafanya uamuzi," alieleza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved