Wachezaji hao ambao wako chini ya uchunguzi wanajumuisha washambuliaji wawili Kylian Mvbappe na Vinicius Junior. Wengine ni pamoja na Dani Caballos na mlinzi Antionio Rudiger.
Tukio hilo ambalo limeanza kufanyiwa uchunguzi lilifanyika wakati timu hiyo ya soka ikiwa ugenini kwa Atletico Madrid.
Wachezaji hao wanne wanadaiwa kufanya ishara kwa mashabiki wa nyumbani baada ya Real Madrid kuwashinda wapinzani wao wa jiji kwa mikwaju ya penalti na kujikatia tiketi yao katika robo fainali.
Picha za televisheni zilionyesha beki wa Ujerumani Rudiger akionekana kufanya ishaya ya kukata koo, inaonekana kuelekea umati baada ya ushindi wa mikwaju, huku Mbappe akionekana kufanya ishara ya kunyakua gongo. 'gesture'
Vyombo vya habari vya Uhispania vilisema kwamba Atletico Madrid iliripoti vitendo hivyo kwa Uefa wiki iliyopita.
Wachezaji hao iwapo watapatikana na hatia wanaweza kuwa katika hatari ya kusimamishwa kucheza kwenye mechi kadhaa lakini hakuna hakikisho kwamba kesi hiyo itasikilizwa kabla ya robo fainali yao na Arsenal.
Mkondo wa kwanza wa mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Emirates mnamo 8 Aprili na mkondo wa marudiano wiki moja baadaye.
Katika taarifa, Uefa ilisema: "Mkaguzi wa maadili na nidhamu ameteuliwa kuchunguza madai ya mwenendo usiofaa" yaliyotolewa na wachezaji wanne wa Real Madrid.
UEFA itachunguza ikiwa ishara za wachezaji hao zililenga moja kwa moja mashabiki wapinzani na ikiwa ni ukiukaji wa Kanuni za nidhamu. Ikiwa watapatikana na hatia ya kukiuka sheria, klabu na wachezaji wanaweza kukabiliwa na vikwazo.
Real Madrid watalazimika kuwatetea wachezaji wake mbele ya UEFA, wakitoa ushahidi wa kuhalalisha tabia zao na kuepuka adhabu zinazoweza kutokea.
Klabu hiyo inasema kuwa sherehe hiyo ilikuwa ya hiari, ikionyesha tu mvutano wa mechi, na haikukusudiwa kuwachokoza wafuasi wa Atlético de Madrid.